Loading...
title : KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA
link : KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA
KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, Sadi Kusilawe amewataka viongozi wa chama hicho kuvunja Makundi na kuacha kabisa swala la maneno ili kufanikisha ushindi wa kishindo katika marudio ya uchaguzi wa Udiwani kata ya Saranga.
Kusilawe amesema hayo alipokuwa anaongea na wajumbe wa halmashauli kuu ya wilaya ya ubungo katika mkutano ulio wakutanisha viongozi hao na kutumia muda huo kuwaasa viongozi hao kuchagua kiongozi bora na atakaye kubalika kwa wananchi ili chama kiweze kupata ushindi wa kishindo kwenye marudio hayo ya uchaguzi.
"uchaguzi ni kama biashara, leo tuko saranga, mmepiga kura za maoni jana, kura zile zitakuja kuwaambia kuwa saranga tunakwenda na kuku au bata , tutakapo kwenda watatuambia , nikimaanisha tunapaswa kumchagua mgombea ambaye anafaa na anauzika kwa kwa jamii , kwani ukiwa umepita na kuku watu watakuuliza hiyo ni biashara ???? Lakini ukibeba bata hakuna atakae kuuliza kwakuwa wanajua unaenda kufuga hivyo hawaulizi bei na sisi tufanye uchaguzi ambao utatupa kiongozi anaye pendwa na kukubalika na jamii na majibu tutapata kesho kutwa" amesema Kusilawe.
Aidha aliwaasa viongozi kuwa na moyo wa kutunza vitu na kulinda sana mdomo kwani wote tunajua mdomo ni jumba la maneno kuna wakati unaweza kuongea kitu ambacho kinajenga au kubomoa, huku akisisitiza kuwa na weledi wa kuchambua mambo punde unapo letewa taarifa yoyote , alizidi kueleza kuwa kiongozi bora hupaswi kuwa na maneno mengi, kiongozi akipenda kuongea sana huyo sio kiongozi bali ni kiwanda cha kuzalisha maneno.
Sambamba na hayo aliwaonya makatibu wa matawi kusimamia vyema vitega uchumi vyote vya chama kwa umakini kwani kuna baadhi ya makatibu wamejibinafsishia vitega uchumi hivyo na kuvimiliki kama vyao kitu ambacho chama hakito kubali wala kufumbia macho vitendo hivyo vya wizi wa mali za chama.
Pia ndg sadi alitumia nafasi hiyo kutoa onyo kali kwa viongozi ambao hawapendi kuvaa sare za chama cha mapinduzi na kuwataka waache mara moja tabia hiyo kwani kwa kufanya hivyo watajikuta kwenye matatizo ya kuitwa kunguru ikiwa na maana ya mamluki wa chama ambao wanavujisha siri za chama na hivyo kujikuta kwenye kashfa zisizo na maana yoyote, alihoji kuwa RAIS na MWENYEKITI wa CCM Taifa mheshimiwa JOHN MAGUFULI anafanya kazi nzuri hivyo hakuna aja ya kukificha chama chako hivyo ni muhimu kwa wajumbe kuvaa sale za chama .
Alimalizia kwa kuwaasa wanachama wa chama hicho kuacha kuvaa nguo zinazo wabana , vimini na nguo ambazo zinaonesha maumbile ya mtu jinsi yalivyo au kuvaa nguo chini ya makalio kwani kufanya hivyo ni kukosa maadili. pia kikao hicho kiliudhuliwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya ubungo , katibu wa chama wilaya ya ubungo , wajumbe wa halmashauli kuu wiaya ya ubungo , madiwani n.k.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Sadi Kusirawe akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Wilaya ya Ubungo.
Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakimsikiliza katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
Kamati ya Watendaji ya CCM wilaya ya Ubungo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi
Hivyo makala KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA
yaani makala yote KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/katibu-ccm-dar-awataka-viongozi-kuvunja.html
0 Response to "KATIBU CCM DAR AWATAKA VIONGOZI KUVUNJA MAKUNDI KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI SARANGA"
Post a Comment