Loading...

UN KUADHIMISHA MIAKA 72.

Loading...
UN KUADHIMISHA MIAKA 72. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UN KUADHIMISHA MIAKA 72., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UN KUADHIMISHA MIAKA 72.
link : UN KUADHIMISHA MIAKA 72.

soma pia


UN KUADHIMISHA MIAKA 72.




Na Noel Rukanuga.
Mwambawahabari
Umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana  na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajia kuadhimisha miaka 72 ya kuanzishwa umoja wa Matifa.

Maadhimisho hayo yanatarajia kufanyika Oktoba 24 mwaka huu Jijini Dar es Salaam katika Viwanja Karimjee, huku kilele chake kinatarajia kufanyika Kisiwa cha Unguja, Zanzibar.

katika Maadhimisho hayo zaidi ya wageni 500 wakiwemo Mabolozi wa nchini mbalimbali,viongozi wa Serikali wataudhuria huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mratibu Mkazi wa UN, Alvaro Rodriquez amesema kuwa  umoja wa mataifa umekuwa ukitekeleza mipango mbalimbali ya kimaendeleo katika kuhakikisha Tanzania inapiga hatua.

Amesema kuwa kwa sasa kuna mradi Mkubwa Mkoa wa Kigoma ambao umefadhiliwa na nchi ya Norway pamoja na KOICO.

Rodriguez amesema kuwa mradi huo umelenga kuchochea maendeleo katika Mkoa wa Kigoma hasa kwa kuzilenga jamii za wenyeji katika Wilaya Tatu ikiwemo Kasulu, Kibondo, Kakonko ambazo kwa pamoja zinawahifadhi zaidi ya Wakimbizi 300,000.

"Tanzania na Umoja wa Mataifa zimekuwa na uhusiano mzuri wa ushirikiano kwa miongo mingi hasa katika kipindi kinachopitia mabadiliko ya kuelekea katika hadhi ya kipato cha kati" amesema Rodriguez.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Dkt. Suzan Kolimba, amesema kuwa uwepo wa umoja wa mataifa hapa nchini kumechangia masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Amesema kuwa kupitia maadhimisho ya miaka 72 ya UN imeweza kuchangia masuala ya kimaendeleo katika kutoa msaada.

Dkt. Kolimba amesisitiza kuwa sekta ya viwanda katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo endelevu.

Hata hivyo amebainisha kuwa maadhimisho ya mwaka huu yamebeba ujumbe unaosomeka 'Maendeleo ya Viwanda na Utuzanzaji Mazingira kwa Maendeleo endelevu'.

Umoja wa  Mataifa ulianza kufanya Kazi Oktoba 24 mwaka 1945 mpaka sasa umetimiza miaka 72 tangu kuanzishwa kwake.


Hivyo makala UN KUADHIMISHA MIAKA 72.

yaani makala yote UN KUADHIMISHA MIAKA 72. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UN KUADHIMISHA MIAKA 72. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/un-kuadhimisha-miaka-72.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UN KUADHIMISHA MIAKA 72."

Post a Comment

Loading...