Loading...
title : Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza.
link : Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza.
Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Temeke,(RCO) kufika mahakamani hapo bila kutoa udhuru, kujieleza kwa nini upelelezi dhidi ya kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mritana mfanyabiashara Revocatus Muyela haukamiliki.
Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema hayo baada ya wakili wa serikali, Patrick Mwita kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua za mwisho kukamilika.
"RCO aje kutueleza mwenyewe hatua ya upelelezi wa kesi hiyo, kwa sababu imekuwa ikiahirishwa kwa mara hakuna excuse" amesema hakimu Simba
Kufuatia agizo hilo kesi imeahirisha hadi October 30/2017.
Washitakiwa Miriam na Revocatus Februari 23, mwaka jana waliachiwa huru mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa mashtaka upya ya mauaji.
Katika kesi hiyo namba 5/2017 wanadaiwa Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Kwa makusudi walimuua Dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.
Hivyo makala Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza.
yaani makala yote Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/kesi-ya-erasto-msuyarco-temeke-atakiwa.html
0 Response to "Kesi ya Erasto Msuya,RCO Temeke atakiwa kufika mahakamani kujieleza."
Post a Comment