Loading...

MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.

Loading...
MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.
link : MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.

soma pia


MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.








Na Ramadhani Ali – Maelezo.
Mwamko mkubwa wa kufanya mazoezi unaonekana sehemu nyingi za Zanzibar bado  haujasaidia sana kupunguza maradhi yasioambukiza na hatimae maradhi hayo yanaendelea kuwasumbua wananchi wengi.

Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Omar Mwalimu alisema hayo kwenye mhadhara wa wazi wa wanafunzi wa vyuo vikuu ulioandaliwa na Mtandao wa Kimataifa wa wananfuzi wa Zanzibar uliofanyika Chuo Kikuu cha Zanzibar Kempasi ya Mpendae.

Alisema kufanya mazoezi ni moja ya sababu ya kupunguza kuongezeka maradhi yasiyoambukiza lakini tatizo ni chakula bora chenye mchanganyiko wa vitu mbali mbali kimekuwa kikikosekana kwa wananchi wengi.

Alisisitiza kuwa kufanya mazoezi kila siku ni jambo la msingi katika kuimarisha afya za wananchi  lakini kuwa muangalifu katika matumizi ya chakula cha kila siku ni kitu muhimu zaidi katika kupambana na maradhi yasiyoambukiza.

Meneja huyo aliwashauri wananchi kubadili tabia na kuwataka kutumia matunda na mboga kwa wingi na kupunguza chakula chenye vichocheo vya kupata maradhi yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiuwa watu wengi zaidi hivi sasa duniani.

Meneja wa Jumuiya ya Muungano wa Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Zuhura Saleh Amour alisema kisukari ambayo ni moja ya maradhi yasiyoambukiza yamekuwa yakipoteza maisha ya wananchi wengi duniani na nchi zinazoathirika zaidi ni nchi zinazoendelea.

Aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu na wananchi wa kawaida kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwani maradhi hayo yanachukua muda mrefu kugundulika kama mtu hajapima afya yake.

Aliwashauri kuacha kutumia bidhaa zinazotokana na tumbaku kwa vile imegundulika kuwa matumizi ya tumbaku ni miongoni mwa mambo yanayohatarisha kupata maradhi yasiyoambukiza.

Aidha a
lisisitiza umuhimu wa kuweka mbele kujikinga na maradhi hayo kwani yanapokupata matibabu yake yanakuwa magumu na yanachukua muda mrefu kuondoka.

Akifungua mkutano huo, Afisa wa kitengo cha maradhi hayo Omar Abdalla alisema Zanzibar imeongeza maradhi ya homa ya ini, maradhi ya kinywa na ajali kuwa ni miongoni mwa maradhi yasiyoambukiza.

Alisema maradhi hayo mapya na yale maarufu ya sinikizo la damu, saratani, kisukari na maradhi yanayoambukiza kwa njia ya hewa yanachukua asilimia 43 ya vifo vyote vinavyotokea Zanzibar.

Wanafunzi walioshiriki mhadhara huo walikishukuru kitengo cha maradhi yasiyoambukiza kwa kuwapa taaluma kubwa ambayo imewawezesha kujuwa sababu na njia ya kujikinga na maradhi hayo.

Waliahidi kuwa  watakuwa walimu wazuri wa kuwaelimisha wananchi wenzao na kuwa mfano wa kuigwa na wananchi wengine katika sehemu wanazoishi ili kuona wanajikinga na maradhi hayo. 


Hivyo makala MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.

yaani makala yote MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/maafisa-wa-jumuia-ya-maradhi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAAFISA WA JUMUIA YA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WATOA TAALUMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU."

Post a Comment

Loading...