Loading...
title : Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira.
link : Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira.
Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira.
Jonas Kamaleki-MAELEZO
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kampuni ya Accaso International Limited, William Kafipa katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.
Kafipa amesema mkaa wa mawe wa kupikia unatumika kwa kiasi kidogo na unawaka kwa muda wa saa nne mfululizo hivyo kuwezesha mtumiaji kupika vitu vingi kwa mkaa kidogo ukilinganisha na mkaa unaotokana na miti.
“Mkaa huu ni bora sana na watu wengi wakiutumia wataachana na kukata miti ovyo hivyo kutunza mazingira na kuepusha nchi kuwa jangwa,”alisema Kafipa.
Aliongeza kuwa badala ya kutumia gunia moja la mkaa wa kuni ambalo gharama yake ni kati ya shilingi 60,000/= na 85,000/=, unaweza kutumia boksi mbili hadi tatu za mkaa wa mawe kwa matumizi sawa na gunia hilo ambayo jumla yake ni shilingi 36,000/=. Kwa kufanya hivyo mtumiaji ataokoa fedha yake na pia atatunza mazingira kwani hatalazimika kukata miti ili kupata mkaa.
Kwa upande wake, Afisa Masoko na Mauzo wa Accaso, Monica Cornelius amesema mkaa wa mawe utampunguzia mwanamke adha ya kutembea mwendo mrefu kutafuta kuni endapo atatumia mkaa huo ambao bei yake ni nafuu hata kwa mtu wa kipato cha chini.
“Mkaa huu hautoi moshi jambo ambalo ni zuri kwa mazingira na kwa kwa afya ya mtumiaji, hii itaepusha pia mauaji ya vikongwe ambao walikuwa na macho mekundu kutokana na kupikia samadi au kuni mbichi,” alisema Monica.Monica ameongeza kuwa akina mama na watu wengine waipokee teknolojia hii mpya ya mkaa wa mawe wa kupikia ili iweze kubadilisha maisha yao.
Hivyo makala Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira.
yaani makala yote Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/matumizi-ya-mkaa-wa-mawe-wa-kupikia.html
0 Response to "Matumizi ya mkaa wa mawe wa kupikia yatapunguza ukataji miti ovyo na kuepusha uharibifu wa mazingira."
Post a Comment