Loading...
title : Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo
link : Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo
Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo
Mashindano ya kumsaka mrembo wa Kiss Universe Tanzania yamepangwa kufanyika leo (Jumamos) kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini. Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 10 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa mujibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Tsehai Sarungi.
Maria amewataja mabondia hao kuwa ni Lilian Maraule , Glory Gideon, Melody Tryphone, Anitha Mlay, Silvia Mkomwa, Rogathe Ally, Prisca Dastan ambao wote wanatoka Dar es Salaam. Warembo wengine ni Maureen Foster na Mary Peter wanaotoka Mwanza wakati anayetoka mkoa wa Mbeya Zahra Abdul. Warembo hao walipata mafunzo mbalimbali katika kambi ikiwa pamoja na mafundisho ya ujasiriamali yaliyoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO) chini ya Mkurugenzi Mtendaji, Jensen Shuma.
Warembo hao walipata ujuzi wa jinsi ya kutengeneza majiko ya kisasa ya kupikia kwa kutumia udongo na bati, jinsi ya kutengeneza majiko ya kuoka keki yenye gharama nafuu, jinsi ya kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba mbalimbali na ujuzi mwingine. Maria alisema kuwa walipata mafunzo hayo kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais upande wa Mazingira ili kuwawezesha warembo kupata ufahamu na kuhamasika kujiajiri ili kujipatia kipato.
“Maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika na wapenzi wa masuala ya urembo watapata burudani safi kutoka kwa DDI Dance, poetry group (Romantic), A beautiful song kutoka kwa Jeff Mduma,” alisema Maria.
Alifafanua kuwa wamedhamilia kumpata mrembo bora ambaye atarejesha heshima ya mashindano hayo kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata ambaye alimaliza katika nafasi tano bora nchini Mexico mwaka 2007.
“Tumefanya uchaguzi wa warembo vizuri na wengi ni bora, kwa sasa tunawafundisha masuala mbalimbali ya urembo, lengo ni kuwafanya wawe bora, wote ni washindi, lakini tunahitaji mshindi mmoja ambaye ataliwakilisha Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” alisema.
Alisema kuwa mashindano hayo pia yatamtoa mshindi wa taji la Miss Earth Tanzania na mshindi wa taji la Miss Tourism Queen International wa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO)Jensen Shuma akielezea warembo wa Miss Universe Tanzania jinsi ya kutengeneza mkaa kwa kutumia pumba na mabaki mbalimbali. Anayefuatilia maelezo hayo ni Mtaalam wa Nishati Endelevu na mabadiko ya Tabia nchi Shima Sango.
Mmoja wa wataalum wa Shirika Lisilo la Kiserikali la TaTedo Eva John aliwaelezea washiriki wa mashindano ya Miss Universe Tanzania jinsi ya kutumia jiko la kisasa la kuoka keki.
Mmoja wa warembo wa Miss Universe Tanzania akitengeneza jiko la kisasa la udongo na bati mara baada ya kupata maelekezo na mmoja wa wataalam wa Taasisi ya Uendelezaji wa Nishati asilia na Uhifadhi wa Mazingira (TaTEDO).
Warembo wanaowania taji la Miss Universe Tanzania 2017, wakiwa katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi ((kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali la (TaTedo) Jensen Shuma na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Martha Ngolowela mara baada ya kutembelea ofisi hizo na kujifunzo ujuzi mbalimbali wa kujiajiriamali.
Hivyo makala Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo
yaani makala yote Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/miss-universe-kufanyika-jumamosi-oktoba.html
0 Response to "Miss Universe kufanyika Jumamosi Oktoba 29, warembo watembelea Tatedo"
Post a Comment