Loading...
title : NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA
link : NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA
NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wakulima na wafugaji wa vijiji vinne alivyotembelea vya wilaya ya Mkuranga kuondokana na tofauti zao na badala yake wapendane.
Hayo aliyasema katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo lake la Mkuranga-Pwani ambapo aliweza kuelezwa kero mbalimbali na kuahidi kuzishughulikia.
Katika ziara hiyo pia aliweza kuchangia jumla ya fedha kiasi cha shilingi Mil.6 pamoja na mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati zilizomo katika vijiji hivyo.
Aidha pia amewaomba wananchi kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali hususani ufugaji wa kuku samaki na mifungo mbalimbali ili kuwawezesha kuondokana na umaskini.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyanduturu akiwa ni ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Nyanduturu kata ya Nyamato ambayo pia amechangia Millioni moja na nusu pamoja na saruji 50 ili kufanikisha ujenzi huo unaoendelea.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni,Mohammed Mpunjika akimkabidhi risala yao Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipofanya ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mmoja wa akina mama kutoka katika kijiji cha Tipo kata ya Nyamato akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya ziara yake .
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga,Ally Mohammed akizungumza jambo.
Muonekano wa jengo hilo.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-ulega-atembelea-vijiji.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI ULEGA ATEMBELEA VIJIJI VINNE VYA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKURANGA"
Post a Comment