Loading...

Bobi Wine kurejea Uganda kesho

Loading...
Bobi Wine kurejea Uganda kesho - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Bobi Wine kurejea Uganda kesho, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Bobi Wine kurejea Uganda kesho
link : Bobi Wine kurejea Uganda kesho

soma pia


Bobi Wine kurejea Uganda kesho

Mbunge wa Kyandodo Mashariki mwa Uganda ,Robert Kyagulanyi ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini humo ajulikanaye kama Bobi Wine anatarajia kurudi nchini Uganda hapo kesho akitokea nchini Marekani ambapo alienda kupata matibabu baada ya kupigwa na vyombo vya dola.
"Nitarejea nyumbani siku ya jumatatu,licha ya kuwa bado nna hofu lakini Uganda ndio nyumbani ambapo familia yangu na watu wangu wapo.Nina wasiwasi lakini waganda milioni 44 nao wana hofu hivyo lazima nirudi," Wine alibainisha hayo wakati akihojiwa na gazeti la Mail na Guardian
"Unaweza kukutana na kitu chochote Uganda,na hata ukiangalia historia ya wapiganaji wengi wa ukombozi wamekuwa wakikamatwa wakati wa ujio wao na mimi sina tofauti na wao hivyo nnatarajia chochote kunikuta wakati nitakaporejea"Bobi Wine alisisitiza.
Wine ambaye aliondoka nchini Uganda mwanzoni mwa mwezi septemba kwa ajili ya matibabu ameeleza pia kuwa ali yake kwa sasa inatengemaa .
Bobi Wine alikamatwa tarehe 13 Agosti baada ya mkutano wa kampeni kaskazini-magharibi kwenye mji wa Arua ambapo kuna madai kuwa msafara wa rais ulitupiwa mawe.
Mwanamuziki huyo mwenye miaka 36 awali alishtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi kwa makosa ya umiliki wa silaha kinyume cha sheria, mashtaka ambayo yalifutwa baadaye. Kisha akafunguliwa mashtaka ya uhaini kwenye mahakama ya kiraia.
"Kwa sababu mimi asili yangu ni Uganda na wala sijatokea katika familia ya hali ya juu kifedha na asili yangu ni mtoto wa mtaani .
Hivyo historia yangu ipo wazi ili kila mmoja aione ,ninapoongea wajione wao pia kwamba nnawakilisha sauti zao kupitie kwangu kwa sababu nnajua maumivu wanayopitia"Wine alitoa ujumbe kwa waganda.
Vilevile Wine alieleza kwamba kipindi atakaporudi Uganda hatasababisha vurugu kutoka kwake au wafuasi wake lakini ataendelea kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya kwa muda wote kwa kuwapa moyo waganda na kila mmoja kufanya jukumu lake na kila mmoja kusimama kudai haki yake


Hivyo makala Bobi Wine kurejea Uganda kesho

yaani makala yote Bobi Wine kurejea Uganda kesho Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Bobi Wine kurejea Uganda kesho mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/bobi-wine-kurejea-uganda-kesho.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Bobi Wine kurejea Uganda kesho"

Post a Comment

Loading...