Loading...
title : NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI
link : NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI
NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI
NEC-DODOMA
Tume ya Taifa ya uchaguzi imesema kuwa Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani wa Kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo (16.10.2017) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Ramadhani Kailima Mjini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasiadizi wa uchaguzi yanayoratibiwa na kuendeshwa na NEC.
Bw. Kailima amesema wapiga kura hao wataruhusiwa kutumia vitambulisho vya uraia vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Hati ya kusafiria na Leseni ya udereva.
“Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia kifungu namba 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambacho kinasema mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari atakwenda mwenyewe kwenye Kata aliyojiandikisha na kituo alichopangiwa” Amesema.
Ameeleza kuwa hatua hiyo ni kumridhisha msimamizi wa kituo au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwamba yeye ndiye mpiga kura halali na kuongeza kuwa kifungu hicho kinamtaka Mpiga Kura aonyeshe kadi yake ya kupigia. Aidha, kinaeleza kwamba Tume inaweza ikaelekeza utambulisho mwingine wowote utakao msaidia mpiga kura kuweza kupiga kura iwapo hana kadi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI
yaani makala yote NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/nec-yaagiza-waliopoteza-vitambulisho_16.html
0 Response to "NEC YAAGIZA WALIOPOTEZA VITAMBULISHO KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WADIWANI"
Post a Comment