Loading...

Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon

Loading...
Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon
link : Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon

soma pia


Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon

SHIRIKA la ndege la Precision Air leo limetangaza udhamini wake wenye thamani ya Sh 20 milioni kwa ajili ya mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 jijini Mwanza.

Kwa udhamini huo, shirika hilo sasa linatambulika rasmi kama shirika maalumu la usafiri wa mbio hizo miongoni mwa wadhamini wengine zikiwemo kampuni za PUMA, Tiper, RedBull, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), New Mwanza Hotel, EF Out door, CF Hospital, KK Security, na kampuni ya uchapishaji ya SDS.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo ,Meneja Masoko na Mahusiano wa Precision Air Bw Hillary Mremi alisema udhamini huo kwa kiasi kikubwa umechagizwa na malengo ya mbio hizo yaliyojikita katika kutangaza utalii wa ndani kupitia mchezo wa riadha.

“Lakini pia kibiashara tunaona kwamba mara nyingi watu wanaopenda kushiriki riadha wamekuwa na ‘hobby’ pia kusafiri sehemu tofauti tofauti ndani na nje ya nchi hivyo ushiriki wetu kwenye mbio hizi utazidi kutukutanisha na kundi hili muhimu,’’ alibainisha.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirikala la Ndege la Precision Air Bw Hillary Mremi (wa pilikushoto) akikabidhi mfano wa tiketi ya ndege kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon, Bw Zenno Ngowi ( wa pili kulia) ikiwa ni ishara ya udhamini wenye thamani ya Sh 20 milioni kwa ajili ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Octoba 29 jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe (wa tatu kushoto) pamoja na maofisa wa makampuni hayo mawili.
Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirikala la Ndege la Precision Air Bw Hillary Mremi akizungumza wakati wa makababidhiano hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi pamoja  na Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi (katikati) akizungumzia udhamini huo. Kwa mujibu wa Ngowi udhamini huo unamaanisha kwamba uhusiano wa Precision Air na wateja wake hautaishia  ndani ya ndege bali utaendelea zaidi hadi kwenye mitaa, fukwe, viwanja vya michezo na sehemu zote za utalii katika jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa yote.
Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus, Bw Bidan Lugoe (katikati) akizungumzia udhamini huo. Kwa mujibu Lugoe maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba wamejipanga kupokea washiriki zaidi ya 4,000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo viongozi na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.



Hivyo makala Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon

yaani makala yote Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/precision-air-yaongeza-nguvu-udhamini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Precision Air yaongeza nguvu udhamini Rock City Marathon"

Post a Comment

Loading...