Loading...

Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki

Loading...
Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki
link : Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki

soma pia


Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati) akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph Kamishina (kulia mbele) katika ziara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Na Greyson Mwase, Geita

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ameitaka Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwasilisha taarifa zote za gharama za uendeshaji wa Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo ili kujiridhisha pamoja na kuchukua hatua za kisheria iwapo kama kuna taratibu za manunuzi zimekiukwa.

Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 27 Oktoba, 2017 alipofanya ziara katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera lengo likiwa ni kufahamu shughuli za migodi ya serikali, binafsi na wachimbaji wadogo.

Alisema kuwa gharama za uendeshaji wa shughuli za mgodi huo zimekuwa ni kubwa mno pamoja na madeni hali inayopelekea shirika hilo kujiendesha kwa hasara badala ya kujiendesha kwa faida.
Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph Kamishina (katikati mbele) akimwongoza Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ( wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kulia) kuelekea kwenye eneo la uchenjuaji katika mgodi huo.

Aliendelea kusema kuwa STAMIGOLD imekuwa ikitumia gharama kubwa sana katika uendeshaji wa shughuli zake kwa kutumia mashine za kukodi na kutaka watendaji wa mgodi huo kuwa wabunifu kwa kuibua mikakati mipya kupunguza matumizi na kuzalisha faida kubwa ili hatimaye waweze kutumia vifaa vyake badala ya kukodi.

“ Ukiangalia gharama inayotumika kukodi mashine za uchorongaji na uchimbaji madini na nyinginezo utabaini kubwa sana ambapo kama STAMIGOLD ingejipanga ingekuwa na uwezo kabisa wa kununa mashine na mitambo yake yenyewe na kuepuka gharama kubwa za kukodi.
Kaimu Meneja Uchenjuaji kutoka Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo, Joseph Kamishina(katikati) akielezea shughuli za uchenjuaji madini zinavyofanyika kwa Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kushoto) katika ziara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo.

Aidha, Waziri Kairuki alielekeza Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na menejimenti ya Mgodi wa STAMIGOLD kuwasilisha mpango wa kibiashara wenye kuainisha gharama za uzalishaji, mapato na faida.

“ Tunataka kuanzia sasa STAMIGOLD uwe ni mgodi wa mfano wenye kuzalisha kwa faida Tanzania, badala ya kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Kairuki. Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki aliutaka Mgodi wa STAMIGOLD kutumia Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kwenye tafiti zake za madini kwa kuwa wakala huo una wataalam na maabara za kutosha.

Alieleza kuwa kutokana na wakala huo kuwa na uzoefu katika utafiti wa madini ni muhimu kwa Mgodi wa STAMIGOLD kushirikiana nao kwenye utafiti wa madini kama njia mojawapo ya kuboresha tafiti zake.
Kutoka kushoto mbele ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Balozi Alexander Muganda, Waziri wa Madini, Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde wakiendelea na ziara katika eneo la Mgodi wa Uchimbaji Dhahabu wa STAMIGOLD – Biharamulo.

Naye Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliitaka STAMIGOLD kuwa wabunifu kwa kufanya utafiti na kubaini maeneo yenye mashapo ya madini ya dhahabu ili kuwa na miradi endelevu ya uchimbaji madini Alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa sekta ya madini inakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, hivyo inaanza na usimamizi wa karibu kwa migodi yote inayosimamiwa na serikali, binafsi na wachimbaji wadogo na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazojitokeza.



Hivyo makala Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki

yaani makala yote Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/takukuru-kuhakiki-matumizi-stamigold.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Takukuru kuhakiki matumizi STAMIGOLD – Kairuki"

Post a Comment

Loading...