Loading...

TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017

Loading...
TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017
link : TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017

soma pia


TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017

Na Salum Vuai, MAELEZO
USHINDI wa kwanza kwa upande wa wanawake na wanaume kwenye mbio za kilomita 10 katika mashindano yaliyoandaliwa na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), zote zimechukuliwa na wakimbiaji kutoka Tanzania Bara.
Katika michuano hiyo iliyofanyika leo ikianzia makao makuu ya KMKM Kibweni mnamo saa 1:10 asubuhi,  na kumalizikia viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, Dickson Marwa kutoka Musoma aliibuka wa kwanza upande wa wanaume baada ya kukimbia kwa dakika  29:52:02.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mkenya Lameck Mwakio aliyetimka kwa dakika 29:52:07, akifuatiwa na Nelson Mbuya aliyepeperusha bendera ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU), ambaye pumzi zake zilimuwezesha kukimbia kwa dakika 29:59:07.
Kwa matokeo hayo washindi hao walizawadiwa medali za dhahabu, fedha na shaba mtawalia.
Mwanadada Sarah Ramadhan kutoka Arusha alifanikiwa kunyakua medali ya dhahabu baada ya kuwatupa wafukuza upepo wenzake kwa dakika 37:18:25, huku Sharo Myryuti (Kenya) akishika nafasi ya pili akikimbia kwa dakika 37:38:43 na kuondoka na medali ya fedha.
Mwanariadha mzoefu wa michuano ya kimataifa Zakia Mohammed Mrisho kutoka Arusha, aliambulia namba tatu akifikisha muda wa dakika 38:43:45 na kutia mikononi medali ya shaba.
 Naibu Mkuu wa KMKM Kapteni Khamis Simba Khamis (suruali nyekundu) akianzisha mbio  za Kilomita 10  (KMKM 10 Km Race) zilizoanzia Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni na kumalizia viwanja vya Maisra Mjini Zanzibar.
 Washiriki wa mbio  za kilomita 10 zinazoandaliwa na KMKM wakianza kukimbiza kupitia mitaa mbali mbali ya Zanzibar baada ya kuzinduliwa na Naibu Mkuu wa Kikosi hicho Capteni Khamis Simba Khamis.
 Washindanaji wa mbio za kilomita 10 wakipita katika mzunguko wa eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar wakielekea viwanja vya Maisara ambapo ndio mwisho wa mbio hizo.
 Mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 10 mwaka 2017 Dickson Marwa kutoka Dar es Salam akimaliza mbio hizo katika viwanja vya Maisara kwa kutumia dakika 29:52.02 akifuatiwa  na Lamek Mwakio kutoka Kenya alietumia dakika 29:52.07. Mshindi wa tatu ni Nelson Prya.
 Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Sara Ramadhani Makera kutoka Arusha akimaliza mbio hizo kwa kutumia dakika 37:18.25, Mshindi wa pili wanawake alikuwa Sharo Myryuti kutoka Kenya alitumia dakika 37:38.43. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


Hivyo makala TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017

yaani makala yote TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/tanzania-bara-yatia-fora-mbio-za-kmkm.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANZANIA BARA YATIA FORA MBIO ZA KMKM 10 KM RACE MWAKA 2017"

Post a Comment

Loading...