Loading...
title : TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA
link : TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA
TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA
Mmoja wa viongozi wa Chama cha watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania(TAS) Rehema Athuman ( kulia) akimjulia hali Mzee Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga, Kata ya Kisaki, wilaya ya Morogoro ambaye alikatwa sehemu ya mkono wake wa kushoto ambaye juzi aliletwa kutoka kituo cha Afya Duthumi na kulazwa hosipitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kuendelea na matibabu zaidi. ( Picha na John Nditi).
Na John Nditi, Morogoro
CHAMA cha watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania(TAS) kimewaomba viongozi wa dini, siasa na wadau mbalimbali kujikita kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kubadili mitazamo na kuacha kuwadhuru wenye ualbino kutokana na imani za kishirikina na wambue nao ni binadamu sawa na walivyo wengine.
Mwenyekiti wa TAS Taifa, Nemes Temba alisema hayo hivi karibuni ( Okt 5) mjini hapa baada ya kumjulia hali mwenzao Nassoro Msingili (75) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nyarutanga, Kata ya Kisaki , wilayani Morogoro mwaka huu baada ya kufanyiwa ukatili Oktoba 3, mwaka huu na baadhi ya watu kumkata mkono wa kushoto na kutokomea nao.
Temba alisema, kitendo cha Mzee Msingili kukatwa mkono kimewaumiza wao kama watu wenye ualbino na taifa kwa ujumla na kukemea vikali kitendo hicho kwa kuwa kufuatia tayari ameongezewa ulemavu mwingine zaidi ya ualbino aliokuwa nao.
Alisema kuwa kwa wastani asilimia kubwa ya suala la mauaji, kukatwa viungo na kunyanyaswa kwa watu wenye ualbino ni ya kishirikina ambao unapaswa kukemewa na kupingwa vita na kila Mtanzania.
Hivyo alimwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kulitolea tamko la kukemea vikali vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino nchini ili waweze kuishi kwa amani sawa na watanzania wengine.
waandishi wa Habari mjini Morogoro juu ya wao kukemea vikali kitendo cha ukatili alichofanyiwa albino mwenzao Nassoro Msingili (75) mkazi wa kijiji cha Nyarutanga Kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro vijijini Oktoba 3 mwaka huu.
“ Natoa wito kwa viongozi wa dini, siasa na wadau mbalimbali washiriki kutoa elimu kwa wananchi ili wabadili mitazamo na kuacha kuwadhuru albino kwa imani za kishirikina na badala yake atambue kuwa albino nao ni binadamu kama walivyo watu wengine” alisema Temba.
Hata hivyo aliiomba Serikali kufanya jitihada kwa kushirikiana na wadau wengine kuweza kupata takwimu sahihi za ualbino ili kuweza kuwalinda na kupatia huduma muhimu .
Msingili (75) alikatwa mkono wa kushoto mnamo Oktoba 3 ,mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika kijiji cha Nyarutanga , kata ya Kisaki, wilayani Morogoro baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana wakati akiwa amelala nyumbani ,na kulazwa katika Kituo cha afya Duthumi ambapo juzi alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Akizungumza na gazeti hili juzi , akiwa wodi ya majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro, Msingili alisema kuwa wakati akivamiwa usiku alikuwa peke yake kwa kuwa ndugu zake walikuwa wamehamishia makazi ya muda shambani kuvuna nafaka.
Alisema kuwa akiwa amelala usiku watu wasiofahamika walimvamia nyumbani kwake na walimpiga na kitu butu kama rungu kichawani na alipojihami kwa kuinua mgomo wake wa kushoto juu ghafla akikatwa na panga na watu hao kutokomea na sehemu ya mkono wake wa kushoto.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Leonce Rwengasira,alisema kufuatia tukio hilo Polisi inawashirikia watu wawili kwa tuhuma hizo ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili upelelezi bado unendelea kufanyika na watafikishwa mahakamani wakati wowote ule.
Hivyo makala TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA
yaani makala yote TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/tas-taifa-waomba-elimu-itolewe-kulinda.html
0 Response to "TAS TAIFA WAOMBA ELIMU ITOLEWE KULINDA WATU WENYE UALBINO VIJIJINI NA MIJINI, ALIYEKATWA MKONO ASIMULIA"
Post a Comment