Loading...

TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga

Loading...
TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga
link : TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga

soma pia


TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga

Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack amezindua rasmi huduma ya TTCL 4G mkoani Shinyanga, na kuitaka kampuni kutoa huduma bora za uhakika na zenye gharama nafuu ambazo Wananchi wa kawaida watamudu.

Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika jana katika ofisi za TTCL, mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba, viongozi wa vyombo vya usalama, viongozi wa Mkoa na Wafanyakazi wa TTCL.

Akizungumza katika hafla hiyo, Telack ameitaka TTCL kuongeza ubunifu na juhudi katika kutoa huduma ili iweze kupambana na ushindani uliopo kwenye soko la mawasiliano. “Soko la huduma za Mawasiliano limepanuka sana hapa Nchini, Watoa huduma wapo wengi, ushindani mkali ambapo kila Kampuni inabuni mbinu za kujitanga ili kuvutia Wateja kwa ofa na zawadi mbalimbali.

"Tunataka TTCL yetu nayo ifanye hivyo, ishindane sokoni, iongoze kwa kuwajali Wateja na kutoa huduma bora za uhakika, zenye gharama nafuu ambazo Wananchi wa kawaida watamudu. Tunahitaji kuona sababu ya msingi ya kutoka huku tulipo na kurejea nyumbani TTCL” amesema Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba amesema kuwa TTCL imekuja Shinyanga kuwapa suluhisho bora la Mawasiliano, huduma bora, gharama nafuu na za uhakika. 

“Tumewafuata Wafanyabiashara wa Madini na Vito vya thamani, tumewafuata Wafugaji wa mifugo aina zote, Wakulima wa Mazao yote ya chakula na biashara, Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa ngazi zote” amesema Bw. Waziri Waziri Kindamba.

Ameongeza kuwa TTCL imeleta huduma ya mawasiliano katika Mkoa wa Shinyanga ili kuongeza ufanisi washughuli za Viwanda, Elimu, Ulinzi na Usalama wa Wananchi kwa ujumla. “Tunataka tuyafikie Makundi yote haya na kuyawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi ili waweze kufikia ndoto na malengo yao pamoja na kuchangia Maendeleo ya Nchi yetu kupitia shughuli zao za kila siku hasa katika kupata taarifa za Masoko na Bei nzuri ya mazao yao. Amesema Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akitoa hotuba katika uzinduzi wa huduma ya TTCL 4G Mkoani humo katika hafla iliyofanyika Oktoba 23, 2017 katika ofisi za TTCL.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba pamoja na Meneja wa Mkoa wa Shinyanga-TTCL, Abdalah Lugage wakishika bango kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL 4G Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TTCL katika uzinduzi wa huduma ya 4G Mkoani humo.



Hivyo makala TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga

yaani makala yote TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/ttcl-yazindua-huduma-ya-4g-mkoani.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TTCL yazindua huduma ya 4G mkoani Shinyanga"

Post a Comment

Loading...