Loading...
title : UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA
link : UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA
UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa itakayotoa huduma za usafirishaji katika Ziwa Victoria.
Akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Profesa Mbarawa, amewataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi ili kazi hiyo ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.
“Mkandarasi ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki wa kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na muda mfupi”, amesema Profesa Mbarawa.Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli ya Mv. Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua zilizofikiwa, na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Bandari ya “Port Bell”, nchini Uganda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mbele), akitoka kuangalia ukarabati wa meli ya Mv. Clarius, katika Bandari ya Mwanza, leo. Meli hiyo inatoa huduma katika visiwa vilivyo kwenye ziwa Victoria.
Muonekano wa Meli ya Mv. Umoja yenye uwezo wa kubeba behewa 22. Meli hiyo inasafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mwanza kuelekea Bandari ya “Port Bell” Uganda.
Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kushoto mbele) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati wa meli katika Bandari ya Mwanza, leo.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa meli ya Mv. Clarius leo katika Bandari ya Mwanza. Kukamilika kwa ukarabati wa Meli hiyo inayotoa huduma katika visiwa vilivyo katika ziwa Victoria kutarudisha huduma za usafirishaji na abiria katika visiwa hivyo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA
yaani makala yote UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/ujenzi-wa-meli-mpya-ziwa-victoria-waiva_31.html
0 Response to "UJENZI WA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAIVA"
Post a Comment