Loading...

MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU

Loading...
MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU
link : MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU

soma pia


MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemkuta mshtakiwa Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scorpion’ anayekabiliwa na shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ana kesi ya kujibu na anatarajiwa kuanza kujitetea, Novemba 14, mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa leo Oktoba 31/2017 na Hakimu Mkazi Flora Haule wa mahakama hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na zaidi ya mashahidi kumi  walioletwa mahakamani pale na upande wa Mashtaka.

Kabla ya kutolewa uamuzi huo, Hakimu Haule alimkumbushia mshtakiwa mashtaka yake. 

Baada ya uamuzi huo kutolewa, mshtakiwa Scorpion amedai kuwa atajitetea kwa kiapo na pia atakuwa na mashahidi wawili ambao walitoa ushahidi upande wa mashtaka.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili Ester Kyala ulipinga hoja hiyo na kudai kuwa mshtakiwa huyo hawezi kutumia mashahidi ambao wamekwisha toa ushahidi wao kwa upande wa Jamhuri na kama anaweza atafute mashahidi wengine.

Kutokana na pingamizi hilo Scorpion amedai atajitetea mwenyewe na pia akaomba mahakama itumie pia ushahidi wa wale mashahidi wawili.

Kufuatia hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi November 14 mwaka huu. Mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kuwa hana makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

Katika kesi hiyo, Njwete anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni  unyang’anyi wa kutumia silaha na kumjeruhi Said Mrisho kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili zikiwemo, tumboni na mabegani na kisha kumtoboa macho kitendo anachodaiwa kutenda Septemba 6, mwaka jana  katika eneo  la Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam.

Pia, anadaiwa kumwibia mali yenye thamani ya Sh 476,000/-. 


Hivyo makala MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU

yaani makala yote MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/mahakama-yamkuta-scorpion-na-kesi-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAHAKAMA YAMKUTA "SCORPION" NA KESI YA KUJIBU"

Post a Comment

Loading...