Loading...
title : UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO
link : UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO
UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO
Na: Veronica Kazimoto.
Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016/17 nchi nzima kuanzia kesho tarehe 3 Oktoba hadi tarehe 3 Novemba, 2017.
Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi watakaokusanya Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo amesema lengo la utafiti huo ni kutoa makadirio ya kiasi cha uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo, mazao yatokanayo na mifugo na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya Tanzania.
"Ningependa kuwasisitizia washiriki kuwa, dhumuni kubwa la utafiti huu wa kilimo ni kutoa makadirio ya uzalishaji wa mazao makuu ya kilimo na maeneo yake yaliyolimwa pamoja na taarifa za mifugo katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", amesema Dkt. Mashingo.
Aidha, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wakuu wote wa kaya watakaochaguliwa kushiriki kwenye utafiti huu, kutoa ushirikiano wa kutosha na hususan kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya uzalishaji wa mazao, huduma zinazotolewa na Maafisa Ugani na aina ya mbegu wanazotumia na kubainisha changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa NBS, Chuo cha Mipango na baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO
yaani makala yote UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/utafiti-wa-kilimo-kufanyika-nchi-nzima.html
0 Response to "UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO"
Post a Comment