Loading...
title : VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO.
link : VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO.
VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO.
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.
Vijana wa kata ya Buza katika mtaa wa Kidagaa wamejitokeza kwenye semina ya mafunzo ya kujiunga na taasisi ya sauti ya vijana (MYIDC) Temeke ili kuepukana na changamoto za kukaa mitaani bila kazi maalumu ya kufanya .
Nae Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite amesema hayo katika semina hiyo iliyofanyika mtaa wa Kidagaa kata ya Buza halmashauri ya Temeke amesema kuwa lego la mafunzo hayo ni kutaka kuwafanya vijana waweze kuunda jukwaa la vijana na baada ya hapo watapatiwa mafunzo kuhusu dira ya vijana na pia lengo likiwa ni kupaza sauti zao katika kuleta maendeleo.
Naye mkazi wa Buza kata ya Kidagaa Fatma Ramadhani amesema kuwa amepata mwamko huo wa kijiunga na taasisi hii ya sauti ya vijana (MYIDC) ili kuepukana na changamoto ya kukaa tu mitaani ameona ni vizuri kutumia fursa zinazotolewa kama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamani ili kujikwamua kiuchumi hapa Nchini.
Mkazi mwingine naye Rajabu Charz amesema kuwa katika mafunzo hayo amejifunza namna ya kutafuta na kuweka mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara na kuondoa woga wa kuthubutu katika kafanya jambo la kuleta mafanikio.
Mwenyekiti Mtendaji MYIDC, Ismae Mnikite akizungumza na waandishi wa habari pamoja na vijana wa mtaa wa Kidagaa kuhusu umuhimu wa mradi wa Sauti ya Vijana (MYID) katika kata ya Buza mtaa wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Muwakilishi wa Diwani kata ya Buza, Mahmoud Rashidi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazowakabili vijana na kujitahidi kujitokeza kwenye shuhuli kama hizi kutokana na kuwa na utayari, pia amewapongeza vijana wa kata hiyo kwa kujitokeza kuhudhuria mafunzo hayo katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkazi wa Buza kata ya Kidagaa, Fatma Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari kususu kuchangamkia fursa na kutoa pongezi za dhati kwa sauti ya vijana MDYDC kwa kuona umuhimu wao kama vijana Taifa la kesho katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini Dar Es Salaam.
Mkazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa, Rajabu Charz akizungumza na waandishi wa habari katika kata ya Buza mta wa Kidagaa Halmashauri ya wilaya ya Temeke akitoa wito kwa vijana wenzake kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza hapa Nchini.
Wakazi wa kata ya Buza mtaa wa Kidagaa waliojitokeza kuhudhuria semina ya mafunzo yaliyotolewa na Mradi wa sauti ya vijana MYIDC ikiwa lengo ni kupata sauti ta vijana pale inapotakiwa kufika ili kuleta maendeleo hapa Nchini.Picha na Agness Francis, Blogu ya Jamii
Hivyo makala VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO.
yaani makala yote VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/vijana-kata-ya-buza-waungana-kupaza.html
0 Response to "VIJANA KATA YA BUZA WAUNGANA KUPAZA SAUTI KATIKA KUJILETEA MAAENDELEO YAO."
Post a Comment