Loading...
title : VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI
link : VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI
VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI
Na Jumia Travel Tanzania
Leo siku ya Oktoba 16 dunia inaadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo Shirika la Chakula Duniani (FAO) kila mwaka huadhimisha kwa shughuli na kauli mbiu mbalimbali. Kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Badili Hali ya Uhamiaji ya Baadaye: Wekeza Katika Usalama wa Chakula na Maendeleo ya Vijijini.’ Kwa mujibu wa FAO, dunia inapitia mabadiliko kadha wa kadha kila kukicha.

Watu wengi wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na sababu tofauti kama vile kuongezeka kwa migogoro na kutokuwepo usalama wa kisiasa. Lakini njaa, umasikini, na kuongezeka kwa matukio ya hali ya hewa yanayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa ni sababu zingine za muhimu zinazochangia katika kupelekea watu kuhama. 
Miongoni mwa changamoto kubwa inayowakumba watu siku za hivi karibuni ni katika upatikanaji wa chakula, matumizi yake na namna ya kudhibiti ili kutoleta athari katika mwili. Kwa kuwa leo ni maadhimisho ya ‘Siku ya Chakula Duniani,’ Jumia Travel ingependa kukushirikisha aina za vyakula vya kupunguza au kuacha kula kabisa kama unataka kupunguza uzito wa mwili wako.
Chipsi. Kwa wakazi wengi wa sehemu za mijini kama vile jiji la Dar es Salaam, chipsi ni mojawapo ya chakula kinachotumiwa na idadi kubwa ya watu. Na hii ni kutokana na upatikanaji wake kwa urahisi karibu kwenye kila maeneo wanapoishi. Kwa mujibu wa tafiti, chakula hiki kinaongeza uzito mwilini kutokana na kuwa na kalori nyingi ndani yake na ni rahisi kuzila nyingi zaidi kwa mpigo. Tafiti pia zinaendelea kwa kuelezea kuwa chipsi pengine ndiyo chakula kinachochangia kuongeza uzito kuliko chakula chochote. Hivyo basi, kwa afya yako unashauriwa kuvichemsha kwa maji na kula badala ya kukaanga.
Vinywaji vyenye sukari nyingi. Vinywaji vinavyotengenezwa na kuongezewa sukari ili kuwa vitamu vinatajwa kuwa ni mojawawapo vyakula hatari zaidi kiafya duniani. Vinahusishwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa uzito na vinaweza kuwa na madhara zaidi mwilini endapo vitatumiwa kwa kiasi kikubwa. Ingawa vyakula hivi huwa na kalori nyingi lakini ubongo wako hauvitambui kama ni vyakula vigumu. Kwa hiyo, kama una nia ya dhati kabisa ya kupungua uzito ni vema ukaachana na vinywaji vya aina hii.
Chokoleti. Inafahamika watu wengi hupendela chokoleti kutokana na utamu wake lakini ni hatari sana kiafya. Hutengenezwa kwa kuongezewa sukari nyingi zaidi, mafuta na unga uliosafishwa zaidi kiwandani kwa kiasi fulani. Chokoleti zina kalori nyingi huku virutubisho vikiwa ni vichache. Kipande cha kawaida cha chokoleti kina kadiriwa kuwa kalori takribani 200-300, huku vipande vikubwa zaidi vinaweza kuwa nazo nyingi zaidi. Lakini kwa bahati mbaya unaweza kukutana na chokoleti karibu kila mahala tena zikiwa zimewekwa kwa kutamanisha zaidi ili kukushawishi kununua. Inashauriwa kama unataka kula chakula kidogo cha kawaida badala yake kula kipande cha tunda au karanga angalau.
Juisi za viwandani. Juisi nyingi za matunda unazoziona madukani zinakuwa na virutubisho vidogo sana ukilinganisha na tunda halisi. Nyingi huwa zinatengenezwa viwandani na kuongezewa sukari. Kiukweli, huwa na sukari nyingi na kalori sawa na soda, tena inawezekana vikazidi. Kwa kuongezea juisi za viwandani hazina nyuzinyuzi ambazo unaweza kuzipata kwenye matunda halisi. Hivyo basi unashauriwa ni vema ukala tunda kamili badala ya juisi kwani faida zake haziwezi katu kulingana kama wengi tunavyoamini.

Hivyo makala VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI
yaani makala yote VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/vyakula-unavyotakiwa-kuepuka-kula-kama.html
0 Response to "VYAKULA UNAVYOTAKIWA KUEPUKA KULA KAMA UNATAKA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI"
Post a Comment