Loading...
title : Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon
link : Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon
Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon
Washindi wa michuano ya Rock City Marathon inayotarajiwa kufanyika Octoba 29 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wanatarajiwa kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 40 pamoja na medali, imefahamika.
Akizungumzia zawadi hizo jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Bidan Lugoe alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi na tano nao pia wakiibuka na zawadi za medali na pesa taslimu.
Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Bidan alisema pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 2/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. Laki 5/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.
“Mbio za kilomita tano tunatarajia kwamba zitaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe, baadhi ya wakuu wa mikoa kutoka kanda ya Ziwa huku pia zikihusisha wadhamini wa mbio hizi kutoka mashirika mbalimabli yaani(Corporates).’’ Alisema.
Aidha wadhamini ambao pia watashiriki katika mbio hizo ni pamoja na kampuni za Tiper, Puma Energy, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, New Mwanza Hotel, Real PR Solutions, Efm Radio, EF Out Door, CF Hospital na Afrimax Strategic Partnerships Limited.
Alibainisha kuwa mbio hizo za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon
yaani makala yote Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/zawadi-za-milioni-40-kushindaniwa-rock.html
0 Response to "Zawadi za milioni 40 kushindaniwa Rock City Marathon"
Post a Comment