Loading...
title : ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU
link : ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU
ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU
Askofu “Atallah Hanna’ ambae ni Askofu Mkuu wa Sebastia wa Kanisa la Orthodox la Kigiriki, amesema: "Uwepo wa Ukristo katika nchi hii takatifu (Palestina), ni uwepo wenye historia ya tangu, kwani Ukristo haukuja Palestina kutoka mahali popote duniani, bali umesambaa kutokea hapa katika ardhi takatifu aliyoichagua Mungu,ili iwe ni sehemu ya upendo wake kwa wanadamu".
Askofu “Hanna”ameongeza kusema kuwa, "Tunatoa wito kwa watoto wetu wasome historia ya kanisa lao na waelewe urithi wao wa kiimani, kibinadamu, kiroho na kiuzalendo. Haifai kuwa hawaelewi historia na mizizi yao ya kina (asili yao) iliyo katika udongo wa nchi hii takatifu. Tunaamini kanisa moja ambalo ni chuo kikuu kitakatifu cha kiutume, lakini pia tunajivunia kuwa sisi ni wana wa nchi takatifu ya Palestina. Tunajivunia kuwa sisi ni wa nchi hii, historia yake, urithi wake na utambulisho wake, huku tukitetea haki ya masuala ya wananchi wake."
Aidha amesema "Katika kumbukumbu ya azimio baya la Balfour, upendeleo wetu utabaki daima na wananchi wa Palestina na kwamba kuvamiwa Palestina kumetokana na azimio la Balfour na wala hakukutokana na Mungu. Hatuwezi kuwakubalia wale wanaomnasibisha Mungu na jambo ambalo sio lake, wala kuwakubalia wale wanaofasiri Biblia kama wapendavyo, hatimae wakasema na kuhalalisha alichokiharamisha Mungu.”
“Tunaamini kwamba Mungu hakuhalalisha mauaji, vurugu, kuhamisha watu kwa nguvu na matendo ya kukiuka Utu na hadhi ya kibinadamu, tunaamini kwamba maadili haya yapo katika dini tatu za kumpwekesha Mungu. Katika imani yetu ya kikristo na kwa mujibu wa maadili yetu ya kiinjili, tunasema haifai kudhulumiwa au kukandamizwa binadamu yeyote, yale yaliyotokea mwaka 1948 ya kuwatoa kwa mabavu Wapalestina katika makazi yao, miji yao na ardhi yao takatifu, sio haki kwa njia yoyote.”
Hivyo makala ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU
yaani makala yote ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/askofu-hanna-nakba-janga-ya-wapalestina.html
0 Response to "ASKOFU HANNA: NAKBA (JANGA) YA WAPALESTINA IMETOKANA NA AZIMIO LA BALFOUR, SIO KUTOKA KWA MUNGU"
Post a Comment