Loading...

DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI

Loading...
DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI
link : DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI

soma pia


DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto amewataka watoa huduma na mafunzo kuhusu lishe bora yaanzie ngazi za shule ya msingi ili kuwajenga watoto kuzingatia mlo bora katika kukuza afya za watanzania. Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).

“Walimu wawe sehemu ya afua za kufundishia wanafunzi juu ya lishe bora hasa kuanzia ngazi za shule ya msingi ili kuwajengea mazoea watoto kupenda kula mlo ulio bora hata wanapokuwa majumbani mwao” alisema Dkt. Ulisubisya. Aidha Dkt. Ulisubisya amesema kuwa baadhi ya watoto walio vijini na mijini wana utapia mlo kwa kukosa chakula kilicho bora hivyo jamii inatakiwa izingatie lishe bora ili kuimarisha afya za watoto nchini.

Mbali na hayo Dkt. Mpoki amesema kuwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawe kipaumbele katika kutoa elimu ya lishe bora ili kuweza kujikinga na Unyafuzi, Kwashakoo na magonjwa yasiombukiza kama vile Kisukari,shinikizo la damu ,magonjwa ya moyo yanayotokana na ulaji kupita kiasi.

Kwa upande wake Meneja wa Magonjwa yasioambukiza ,Usalama wa Chakula na lishe ECSA Bi. Rosemary Mwaisaka amesema kuwa wameamua kuandaa vitini na vitita vya kufundishia lishe bora ili kuweza kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kufikisha elimu hiyo kwa walengwa.

“Tumeamua kuandaa vitini hivi ili viweze kutoa elimu bora kwa watendaji na wahudumu ngazi ya jamii ili kuweza kuwafundisha wanajamii juu ya umuhimu wa kula mlo bora na vitatumika Kenya,Uganda na Tanzania” alisema Bi. Mwaisaka. Mbali na hayo Mshiriki wa Mafunzo ya Lishe bora kutoka ECSA ambae pia ni Mtoa huduma Bi. Evelyne Minja amesema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kutoa huduma katika jamii kuhusu mlo bora hasa kwa watoto vijijini na mijini.

“Mafunzo haya yametufanya tujue jinsi ya kuwahudumia na kutoa ushauri juu ya mlo bora hasa kwa watoto wenye viashiria vya utapia mlo kwa kuwapima na kuwapangia vyakula vinavyostahili” alisema Bi. Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wadau mbalimbali wa maswala ya lishe hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kushoto akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vincent Assey wa kwanza kulia wakati wa uzinduzi wa hivyo vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA).
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akikata keki kuashiria kuzindua vitini vya mafunzo juu ya lishe bora katika jamii yetu vilivyoandaliwa na Kanda ya mashariki ya kati na kusini inayojihusisha na maswala ya afya (ECSA) wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Afisa msaidizi wa ECSA Bi. Dorin Marandu.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya kulia akimlisha keki mmoja wa washiriki na mtoa huduma wa lishe ngazi ya jamii Bi. Evelyne Minja wa pili kushoto wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam. PICHA NA ALLY DAUD -WAMJW.


Hivyo makala DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI

yaani makala yote DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/dkt-mpoki-asisitiza-mafunzo-ya-lishe.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT MPOKI ASISITIZA MAFUNZO YA LISHE BORA YAANZIE SHULE ZA MSINGI"

Post a Comment

Loading...