Loading...

DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR.

Loading...
DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR.
link : DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR.

soma pia


DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR.

Mwambawahabari
Jumuiya ya watanzania wanaoishi Diaspora (Marekani) ijulikanayo kama  Sixth Region Diaspora Caucus Washington kwa pamoja wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mh Paul Makonda  kutatua changamoto za ofisi za walimu wa mkoa huu kwa kutoa makontena 36 ya samani mbalimbali zikiwemo  viti vya kisasa zaidi ya 5000,meza za umeme 2500,meza za kawaida 2500,makabati ya vitabu makubwa 1300 na bao (writing boards) za kuandikia 700.

Mchango huu wa samani ambao una thamani ya zaidi ya dola za kimarekani  $ 800,000  ambazo ni sawa na  shilingi 1,800,000,000 za kitanzania utatumika katika ofisi mpya 402 za walimu zilizoanza kujengwa kupitia kampeni iliyoanzishwa na  Mh Paul Makonda mapema Agosti mwaka huu.

Kupitia samani hizi adhma ya  Mh Paul Makonda  ya kutengeneza mazingira rafiki ya utoaji wa elimu kwa walimu wa Mkoa wa Dar es salaam itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na matarajio ya kupandisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kufikiwa kama matokeo ya miundo mbinu rafiki kwa wote.

Makontena hayo yanatarajiwa kufika nchini mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Mh Makonda amewashukuru wadau hawa ambao bila kuzingatia umbali waliopo na nchi yao bado wameonyesha hari ya kuguswa na changamoto za watanzania wenzao hapa nchini, na kutoa rai kwa watanzania wengine kuendelea kuunga mkono kampeni hii ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es salaam kwa namna watakavyo weza kwani hatma ya ustawi wa maendeleo ya Tanzania ni wajibu wa kila mtanzania.

Imetolewa na kitengo cha habari na uhusiano,ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam.


Hivyo makala DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR.

yaani makala yote DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/diaspora-waguswa-na-kampeni-ya-ujenzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DIASPORA WAGUSWA NA KAMPENI YA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR."

Post a Comment

Loading...