Loading...
title : Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu.
link : Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu.
Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati akiwahamasisha wakazi wa Dar es Salaam kufika katika mbio za Kigamboni Marathon.
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile, awataka wakazi wa wilaya ya Kigamboni pamoja na wananchi wengine kutoka maeneo mbali mbali kujitokeza kwa wingi katika kushiriki tamasha la Mbio la Kigamboni Marathon, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kwa Kigamboni.
Dkt. Ndugulile amesema hayo leo katika Ofisi zake Jijini Dar Es Salaam kuwa mbio hizo ambazo huleta manufaa kwa mwanadamu ambazo hujenga afya na mwili pamoja na kukutana na watu mbali mbali wapya na kubadilisha mawazo ili kuleta mafanikio katika Wilaya hiyo mpya. amesema mbio hizo za Kigamboni Marathoni zitafanyika siku ya jumamosi Disemba 2 mwaka huu kuanzia saa 12 asubuhi katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mbio hizo zenye kilomita 21,10 hadi 5 zitakazoanzia darajani,feri kuelekea kibuguni hadi kumalizikia katika ofisi za afisa wilaya ya kigamboni .
Pia amemalizia kwa kusema kuwa wanachi waendelee kujitokeza katika zoezi zima la kujaza fomu ambazo zinapatikana katika ofisi za Mkuu wa wilaya wa Kigamboni ili kushiriki mbio hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile akipokea fulana kw ajili ya kushiriki Mbio za Kigamboni Marathoni
Hivyo makala Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu.
yaani makala yote Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/dkt-ndugulile-kushiriki-mbio-za.html
0 Response to "Dkt. Ndugulile kushiriki mbio za Kigamboni Marathoni, Disemba 2 Mwaka huu."
Post a Comment