Loading...
title : HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA
link : HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA
HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati wa kikao cha tatu cha mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesisitiza kwamba vyombo vya dola vya ndani ya nchi havijashindwa kuchunguza matukio ya kihalifu yaliyotokea nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuwa na subira.
Amesema Serikali hairidhishwi na matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa, ambayo yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini na baadhi yake yamesababisha vifo na wengine kujeruhiwa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 9, 2017) wakati akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma.
Bw. Mbowe alitaka apew kauli ya Serikali juu ya hatua zilizochukuliwa kuhusu tukio la kushambuliwa na mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu, ambapo alishauri uchunguzi huo ufanywe na vyombo vya kimataifa, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa na vyombo vya ndani vya dola.
“Vyombo vya ndani vya dola vina uwezo mkubwa wa kusimamia usalama wa nchi na vinaendelea na uchunguzi wa matukio hayo yaliyofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa letu. Nawaomba wananchi waendelee kuwa na imani na vyombo vyetu vya dola na mara uchunguzi utakapokamilika taarifa itatolewa.”
Hivyo makala HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA
yaani makala yote HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/hatujashindwa-kuchunguza-matukio-ya.html
0 Response to "HATUJASHINDWA KUCHUNGUZA MATUKIO YA KIHALIFU-MAJALIWA"
Post a Comment