Loading...
title : KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI
link : KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI
KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.
Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni imekuwa kinara wa kuwawezesha wanawake kiuchumi katika vikundi vya uzalishaji mali katika halmashauri zao.
Hayo yamebainika katika utoaji wa tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi katika kwa kutenga asilimia tano (5) katika Bajeti ya mapato ya Halmashauri katika Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi fedha inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akitoa tuzo hizo Mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewapongeza washindi wote waliofanikiwa kutekeleza mpango wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwatengea asilimia 5 katika Bajeti ya mapato ya halmashauri.
Ameongeza kuwa njia pekee ya kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda ni kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani wengi wao wanashiriki katika shughuli za kijasilia mali ambazo zinawapa uwezo wa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali na uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka katika Mikoa na Halmashauri nchini kabla ya kutoa Tuzo kwa Mikoa na Halmashauri zilizofanya vizuri katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akizungumza na Maafisa maendeleo ya Jamii katika siku ya ufungaji wa Mkutano wa 12 wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii na kuwasisitiza kuwajibika na kujituma katika kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akimkabidhi tuzo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Esterine Sephania kwa niaba ya Halmashauri ya Kigamboni iliyoibuka kinara wa uwezeshaji wanawake kiuchumi kupitia mchango wa asilimia 5 katika mfuko wa maendeleo ya wanawake.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI
yaani makala yote KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/kigamboni-kinara-uwezeshaji-wanawake.html
0 Response to "KIGAMBONI KINARA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI"
Post a Comment