Loading...
title : MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV)
link : MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV)
MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV)
Mhe. Jenista Mhagama |
Mikoa yote nchini imeagizwa kuwapima wananchi wake, virusi vya ukimwi (HIV) bure kwenye wiki ya kuadhimisha siku ya ukimwi.
Wiki hiyo inaanza Novemba 24 na kuisha siku ya kilele cha Siku ya ukimwi duniani Desemba Mosi. Kauli mbiu ni “Changia mfuko, okoa maisha, Tanzania bila Ukimwi inawezekana”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hayo jana.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Dar es Salaam. Aliagiza kupatikana wataalamu wa kutosha kwa kila mkoa kwa upimaji huo na ushauri nasaha.
Alisema katika wiki hiyo, kutazinduliwa Ripoti ya utafiti wa kitaifa wa virusi vya Ukimwi, utafiti ambao hufanyika kila miaka minne. Alitaja shughuli nyingine ni uzinduzi wa mkakati wa kondom wa kitaifa, kongamano la kitaifa la wataalamu watakaojadiliana kukabili Ukimwi na huduma ya kupima kwa hiari.
Chanzo-Habarileo
Hivyo makala MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV)
yaani makala yote MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV) Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV) mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mikoa-yote-tanzania-yaagizwa-kupima.html
0 Response to "MIKOA YOTE TANZANIA YAAGIZWA KUPIMA WANANCHI VIRUSI VYA UKIMWI (HIV)"
Post a Comment