Loading...
title : Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande
link : Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande
Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Ikiwa ni mwaka mmoja na nusu sasa tangu kufikishwa mahakamani kwa aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili upande wa mashtaka umeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa shauli hilo bado haujakamilika.
Kitilya pamoja na aliyekuwa miss Tanzania mwaka 1996, ambaye pia alikuwa Ofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa Mara ya kwanza April 1, mwaka jana wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa USD Mil.6
Mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kesi hiyo leo Novemba 3 ilifikishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameileza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Alidai kuwa bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka nchini Uingereza na kuomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi November 10, mwaka huu.
Katika kesi hiyo, washtakiwa wote wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya March 2013 na September 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni kwa serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.
Pia wanadaiwa kuwa March 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani 6 milioni, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.
Hivyo makala Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande
yaani makala yote Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/mwaka-mmoja-na-nusu-sasa-kitilya-na.html
0 Response to "Mwaka mmoja na nusu sasa, Kitilya na wenzake waendelea kusota rumande"
Post a Comment