Loading...
title : Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora
link : Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora
Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora
Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
Mtandao wa Policy Forum( PF) ambao umetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 ambapo ilianza kutumia dhana ya ufuatiliaji wa uwajibikaji jamii ( Social Accountability Monitoring) wameungana na wadau katika mkutano wa kujadiliana mafanikio, changamoto pamoja na mafunzo kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotumi dhana hiyo hapa nchini.
Akizungumza hayo leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Kaimu mwenyekiti Mtandao wa Policy Forum ( PF), Herbon Mwakagenda amesema kuwa lengo hasa la mkutano huo ni kuboresha mbinu zinazotumika na wadau pamoja na kuangalia mafunzo ambayo yanaweza kutumika kwa ujumla ikiwemo pia kutoa pongezi kwa wananchi kwa kuwa na muamko mkubwa wa kufatilia haki zao katika mashirika mbalimbali ya Umma.
Nae pia Mratibu wa mtandao wa Policy Forum (PF), Semkae Kilonzo amezungumzia lengo kuwa ni kutaka kubadiilishana uzoefu na taasisi mbalimbali ili kuweza kuboresha zaidi uchechemuzi wa kutekeleza miradi yao hapa nchini.
Vile vile Mwenyekiti Mwakagenda aliongezea hasa kwa kuzungumzi a changamoto zinazo wakabili wakati wa kufikisha ujumbe kwenye Halmashauri mbalimbali kutokana na ubadilishwaji wa viongozi wa halmashauri hizo na kusababisha taarifa kuchelewe kufika kama inavyotakiwa.
Diwani Kiteto Manyara,Paulo Tunyon ametoa pongezi za dhati kwa wadau wa mtandao wa Policy Forum( PF) kwa kuweza kupeleka mabadiliko Vijijini kwa kukabiliana na changamoto hizo kutokana na uwelewa mdogo wa wananchi hao..
Kaimu mwenyekiti Mtandao wa Policy Forum( PF), Herbon Mwakagenda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtandao huo jinsi unavyofanya kazi na wadau wa Taasisi mbalimbali hapa nchini leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere .
Mratibu wa mtandao wa Policy Forum ( PF), Semkae Kilonzo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna watakavyoweza kukabiliana na changamoto ili kufikia malengo ya juu zaidi wanayokusudia leo Jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere
Wadau wa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere
Hivyo makala Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora
yaani makala yote Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/policy-forum-wajenga-uhusiano-mzuri-na.html
0 Response to "Policy Forum wajenga uhusiano mzuri na Serikali katika kuboresha utawala bora"
Post a Comment