Loading...

Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana.

Loading...
Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana.
link : Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana.

soma pia


Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana.

 Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya katika mwaka 2016 imetoa jumla ya Hekta 271,882.86 za ardhi kwa  vijana nchi nzima ili kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujipatia ajira.

Hayo yameelezwa leo, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Anthony Mavunde  alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Mhe. Aida Khenan juu ya mpango wa Serikali kwa vijana wanaomaliza shule za msingi, Sekondarii na Vyuo kwa kuwazesha kujiajiri.

 “Serikali imeendelea kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao unalenga kuwasaidia vijana wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kuweza kujiajiri kwa kuwapa mikopo ya masharti nafuu na mafunzo ya ujasiriamali,” alisema Mavunde.

Aliendelea kwa kusema, katika kipindi cha mwaka 2013/2014 hadi 2016/17, Serikali kupitia mfuko wa Maendeleo ya vijana imetoa mikopo ya masharti nafuu ya Shilingi Bilioni 5.8 kwa vikundi vya vijana 6,076 vyenye wanachama 30,380 katika Halmashauri za Wilaya 157 kupitia SACCOS za Vijana.

Aidha Mavunde amesema, kupitia programu ya kukuza ujuzi wa  nchi Serikali imeanzisha utaratibu maalum wa kutambua ujuzi uliopatikana kupitia mfumo usio rasmi na kuurasimisha kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wale walio tayari kuhitaji na kuwapa vyeti vinavyotambulika.

“Utaratibu huu unawapafursa vijana wetu ya kuendelea na mfumo rasmi wa mafunzo na pia kutambulika na waajiri au watoa kazi,” alifafanua Mavunde.Vilevile amesema, Serikali imerahisisha utaratibu wa uundaji wa Makampuni kupitia BRELA hivyo vijana wengi wanaomaliza vyuo kuweza kuanzisha Makampuni na biashara zinazowezesha kuajiri vijana wengi.

Hata hivyo, Mavunde amewataka vijana wanaomaliza shule za msingi na sekondari kujiunga katika vikundi vya kuzalisha mali na kusajiliwa rasmi kupitia sheria ya usajili wa NGO’s.Aidha mpaka sasa jumla ya vikundi vya vijana vya uzalishaji mali 10, 200 vimesajiliwa.


Hivyo makala Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana.

yaani makala yote Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/serikali-imetoa-hekta-27188286-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Serikali Imetoa Hekta 271,882.86 kwa Ajili ya Shughuli za Vijana."

Post a Comment

Loading...