Loading...
title : TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark
link : TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark
TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark
Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark, ambao unatarajiwa kuondoa kwa kiasi kikubwa tatizo la upatikanaji wa mbolea hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa nyaraka za usajili wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geoffrey Mwambe amesema Mradi huo wa kimkakati unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa katika ukuaji wa sekta ya viwanda na kwamba TIC inatarajia kuwa mradi huo utaleta kasi ya maendeleo na kukuza sekta mbalimbali, kwani mradi huo ni mkubwa na wenye thamani ya dola bilioni moja nukta tisa za kimarekani.
Mwambe aliongeza kuwa mradi huo ni mafanikio makubwa ya Kituo cha Uwekezaji na unatarajia kuongeza wigo wa ajira hapa nchini kwani utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 4500 kwa Watanzania na kuleta chachu katika ukuaji wa sekta ya viwanda haswa uzalishaji wa mbolea ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ni changamoto kwenye ukuaji wa sekta ya kilimo ambapo watanzania wengi wamejiariri.
Katika halfa hiyo fupi ya makabidhiano, Wilfread Wineam ambaye ni Msimamizi wa mradi huo hapa nchini amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mbolea kiasi cha tani milioni moja nukta tatu kwa mwaka na kitauza karibu asilimia 30 ya mbolea hiyo hapa nchini na inayobaki kuuzwa nje ya nchi.
Naye Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Detlet Waecheter ameishukuru TIC kwa makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa kuhusu mradi huo na amesema anatarajia mradi huo utakuwa ni kivutio kwa makampuni mengine makubwa ya Kijerumani kuweza kuja kuwekeza hapa nchini.
Balozi huyo ameahidi kuleta ujumbe mkubwa wa wawekezaji hivi karibuni kutoka jimbo la Bavaria ili waje hapa nchini kujionea fursa mbalimbali. Mradi huo utasajiliwa hapa nchini kwa jina la Tanzania Mbolea Petrochemicals yaani TAMCO
Hivyo makala TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark
yaani makala yote TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/tic-yafanikiwa-kupata-uwekezaji-kutoka.html
0 Response to "TIC yafanikiwa kupata uwekezaji kutoka kwa makampuni makubwa duniani ya Ferrostaal ya Ujerumani na Haldor Topsoe ya Demnmark"
Post a Comment