Loading...
title : Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini.
link : Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini.
Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ametoa wito huo Novemba 16, 2017 Jijini Dar es Salaam alipokutana na Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke na ujumbe alioambatana nao Wizarani hapo kutoka kwenye Ubalozi huo ili kujadiliana masuala mbalimbali ya madini ikiwemo fursa za uwekezaji.
Waziri Kairuki alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za madini na hivyo zipo fursa lukuki za uwekezaji ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za nchini China kwa manufaa ya pande zote mbili.
“Rasilimali za madini ni nyingi na hivyo zipo fursa mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa na kampuni za China na wakati huo huo kuchangia katika uchumi na pato la Taifa kwa ujumla,” alisema Waziri Kairuki.
Waziri Kairuki vile vile alisema yapo maeneo ambayo wawekezaji wanaweza kushirikiana na Serikali ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni uchimbaji wa madini kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), tafiti za utambuzi wa maeneo yenye madini kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo cha Madini (MRI).
Aidha, aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha madini yanayochimbwa nchini yanaongezwa thamani kabla hayajasafirishwa ili kukuza uchumi wa Taifa na wakati huo huo, kuongeza mapato ya Serikali na kuzalisha ajira zaidi.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke na ujumbe alioambatana nao (hawapo pichani) walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (kulia) akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala mbalimbali.
Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (kulia) akiwa na ujumbe wake kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania walipomtembelea Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (hayupo pichani) ili kujadili masuala mbalimbali ya Sekta ya Madini.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (wa pili kutoka kulia) akijadiliana jambo na ujumbe kutoka Ubalozi wa China nchini ulioongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke (katikati).
Hivyo makala Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini.
yaani makala yote Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/serikali-yawakaribisha-wawekezaji.html
0 Response to "Serikali Yawakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya madini nchini."
Post a Comment