Loading...

SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436

Loading...
SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436
link : SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436

soma pia


SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436

Dares Salaam, Novemba 14, 2017: Sweden imeipatia Tanzania Msaada wa jumla ya Fedha ya Sweden SEK. Bilioni 1.64 ambayo ni sawa na takribani Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu. 

Makubaliano ya msaada huo yamesainiwa Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting.

Bw. James alisema kuwa imesainiwa Mikataba mitatu ya msaada huo ambayo ni; mkataba kwa ajili kusaidia Bajeti ya Serikali wa kiasi cha SEK milioni 600 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 159.59 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2019/2020, ambapo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 watatoa takribani Sh. bilioni 53.20.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kuboresha uhalisia wa Bajeti ili kuweza kutimiza majukumu ya kisera, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kikodi na yasiyo ya kodi na pia kusaidia Serikali kutoa huduma nzuri kwa wananchi kupitia taratibu za manunuzi. 

Mkataba mwingine ni kwa ajili ya kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (EPforR) wa kiasi cha Fedha ya Sweden SEK milioni 885 ambayo ni sawa na Sh. bilioni 235.40 kuanzia mwaka 2017/18 hadi 2020/2021.

“Lengo la msaada huu ni kusaidia Mpango wa Elimu kwa Matokeo ambapo tunapimwa namna ambavyo tumeweza kutimiza wajibu wetu tuliojiwekea katika bajeti. Baada ya ya Serikali kutimiza wajibu wake wa kupeleka fedha katika Sekta ya Elimu kwa wakati, wameamua kutupatia fedha hizo ambazo Serikali tunazipangia kazi kulingana na vipaumbele”, alieleza Bw. James.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia)na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakisaini Makubaliano ya Msaada wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo wa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Ulf Kallsting (kushoto) wakiwa wameinua juu Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa waandamizi kutoka Ubalozi wa Sweden Nchini Tanzania wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Msaada wa wa jumla ya Sh. bilioni 435.79 kwa ajili ya Msaada wa kibajeti na kusaidia mpango wa elimu, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436

yaani makala yote SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/sweden-yaipatia-tanzania-msaada-wa_14.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SWEDEN YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA KIBAJETI SHILINGI BILIONI 436"

Post a Comment

Loading...