Loading...
title : “TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA
link : “TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA
“TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA
JUMUIYA wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) wameiangukia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu (HESLB) kuharakisha fedha za wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo kwa kupata alama D waliopovyuoni(supplementary).
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Stanslaus Kadugalize wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema idadi ya wanafunzi waliofeli baadhi ya masomo vyuoni ni kubwa na mpaka sasa hawajapata fedha za kujikimu .
Alisema fedha hizo ni kama kauli ya Naibu Waziri wa Elimu alivyosema kuwa ifikapo ijumaa wiki iliyopitia fedha ziwe zimefika vyuoni lakini mpaka sasa fedha hizo hazijafika jambo ambalo linawapa wakati mgumuwanafunzi hao.
Mwenyekiti huyo alivitaka vyuo visiweke sababu zisizo za msingi juu ya kuwapa wanafunzi fedha zao za kujikimu kwa wale ambao tayari fedha zimekwisha fikishwa vyuoni kwa kigezo cha kujisajili.
“Tunatambua umuhimu wa kujisajili ila vyuo vitambue pia kwamba wapo wanafunzi wengi wanategemea fedha hizo hizo za bodi ya mikopo (HESLB) ili kulipia gharama za kujisajili kuweza kukamilisha zoezi lakujisajili hivyo vyuo viache kuweka sababu zinazopelekea usumbufu kwa wanafunzi “Alisema.
Kuhusu zoezi la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza alisema sasa bodi ya hiyo imekwisha kutoa kwa wanafunzi 29,000 kwa wale wote ambao wanasifa na hawajapata katika upangaji wa awalialiwashauri kutumia dirisha la rufani linalofunguliwa Novemba 13 mwaka huu ambapo rufaa hizo itakuwa ni bure.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo hakisita kuzungumzia kuhusu zoezi la udahili ambapo ambapo aliitaka TCU kuingilia kati kwani bado kuna usumbufu mkubwa wa wanafunzi wanaoupata na una hatarisha baadhi yaokukosa nafasi ya kusoma.
Hivyo makala “TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA
yaani makala yote “TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala “TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/tahliso-yaiomba-heslb-kuharakisha-fedha.html
0 Response to "“TAHLISO YAIOMBA HESLB KUHARAKISHA FEDHA ZA WANAFUNZI VYUONI”-MWENYEKITI WA JUMUIYA"
Post a Comment