Loading...
title : TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo
link : TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo
TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuanzia tarehe 24/11/2017 hadi 25/11/2017 limeendesha zaoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Songo Songo ambao wamekuwa wakilazimika kusafiri zaidi ya masaa mawili kufuata huduma ya vipimo hivyo katika Hospitali ya Kilwa kivinje.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni Tanzu ya TPDC inayosimamia uendesheshaji na utunzaji wa Miundombinu ya Uchakataji na Usafirishaji wa Gesi Asilia inayoitwa GAS COMPANY (GASCO) Mhandisi Baltazari Mrosso wakati wa ufungaji wa zoezi hilo ameeleza kuwa ni wajibu wao kama Shirika kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuboresha maisha ya Wananchi wa Songo Songo ambao pia ni tegemeo kubwa katika shughuli zinazofanywa na Shirika kuanzia kwenye uzalishaji wa gesi visimani, uchakataji kiwandani na usafirishaji.
Diwani wa Kata ya Songo Songo Mh. Said Mwinyi akifungua rasmi zoezi la upimaji kwa kukipatiwa huduma ya upimaji wa Shinikizo la Damu kutoka kwa Daktari Octavian Modest.
“Sisi kama Shirika la Umma ambalo limewekeza katika Kisiwa hiki katika shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia tunao wajibu wa kushirikiana na wananchi pamoja na uongozi wa Songo Songo ili kuboresha maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi, kuboresha uhusiano na kuendelea vyema na shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia na hivyo leo hii tunahitimisha zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi wa Songo Songo pamoja na kukabidhi vifaa tiba vya upimaji wa ugonjwa wa Kisukari ambavyo hapo awali havikuwepo.” Alieleza Kaimu Meneja Mkuu GASCO.
Daktari wa TPDC, Octavian Modest akimtibu moja ya Wazee wa Kijiji cha Songo Songo waliojitokeza katika zoezi la upimaji wa Afya liloratibiwa na kufadhiliwa na TPDC.
Hivyo makala TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo
yaani makala yote TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/tpdc-laendesha-zoezi-la-upimaji-afya.html
0 Response to "TPDC laendesha zoezi la Upimaji Afya kwa Wananchi wa Songo Songo"
Post a Comment