Loading...
title : VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA
link : VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA
VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA
Na Dotto Mwaibale, Sikonge Tabora
WANAFUNZI wilayani Sikonge mkoani Tabora wataanza kunufaika na viazi lishe baada ya kupokea mbegu bora ya viazi hivyo, mihogo na mahindi ya Wema kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB)
Hayo yameelezwa katika Kijiji cha Kisanga na Mkuu wa Wilaya hiyo, Peres Boniface Magiri wakati akizungumza na wakulima kwenye uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazilishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga.
Magiri alisema baada ya kuotesha mbegu hiyo ya viazilishe kwa wingi kitakachofuata ni kuanzisha utaratibu wa wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya hiyo kupata chakula cha mchana badala ya kwenda nyumbani.
Alisema wilaya hiyo kupelekewa mbegu hizo kwao ni fursa kubwa na kwa kushirikiana na wakulima na maofisa ugani atahakikisha mashamba darasa hayo yanatunzwa na kutoa mrejesho.
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa COSTECH, Audax Mutagwa (kulia), akimkabidhi mbegu ya mahindi aina ya Wema, Mkuu wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Peres Boniface Magiri wakati wa uzinduzi na kukabidhi mbegu bora za Mahindi ya Wema 2109, mihogo na viazi lishe kwa ajili ya mashamba darasa katika vijiji vya Isunda, Kisanga, Udongo na Kanyamsenga wilayani humo jana.
Wanakikundi cha Aliselema wakishusha mbegu ya mihogo tayari uzinduzi wa shamba darasa.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza kabla ya kuanza uzinduzi huo katika Kijiji cha Isunda kilichopo Kata ya Nkolye.
Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Maruku kilichopo mkoani Kagera Jojianas Kibura akielekeza namna ya kupanda mihogo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA
yaani makala yote VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/viazi-lishe-kutolewa-kwa-wanafunzi.html
0 Response to "VIAZI LISHE KUTOLEWA KWA WANAFUNZI SIKONGE MKOANI TABORA"
Post a Comment