Loading...
title : Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8
link : Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8
Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8
Vikundi vya VICOBA 272 vya mikoa ya Kanda ya Ziwa vimenufaika na uwezeshaji wa mikopo ya Tsh. bilioni 2. 8 toka Benki ya Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance PLC ili wanachama wake waweze kuitumia katika shughuli za ujasiriamali na kushiriki katika uchumi wa taifa lao.
Vikundi vya VICOBA vilivyo nufaika na mikopo hii vinatoka katika Wilaya au halmashauri za Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu na Mara kwa lengo la kuviwezesha viweze kushiriki katika kuondoa umasikini miongoni mwa wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo hiyo mkoani Geita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama alisema mkopo huo ni sehemu ya Uwezeshaji wananchi kupitia vikundi vya ViCOBA ili waanzishe au waimarishe miradi yao ya ujasiriamali.
‘’Huu ni uwezeshaji Mkubwa na tunataka mkatumie fedha hizi kuendeleza miradi yenu ya ujasiriamali ili ikazalishe na muweze kuondokana na hali duni ya vipato,” na hiyo pia itawasaidia kushiriki katika uchumi wa nchi,aliongeza kusema,Bi Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu,Bi. Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa FERUSCO Sustainable Development,Bw. Felisi Ngonyani mbele mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.2 wakati wa uzinduzi wa utoaji mikopo katika mikoa ya kanda ya ziwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi. Beng’i Issa wapili kulia, Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa tatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na Mbunge, Bw. Joseph Musukuma kulia na Meneja Tawi TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bi. Jenista Mhagama wa tatu kulia akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Mtandao wa ViVOBA Endelevu (Visudent) Kamara Mohamed kulia, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taiifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wa pili kulia, Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bw. Robert Lughumbi wa watu kushoto, Meneja Tawi TPB Mwanza, Bw. Shaban Telatela kushoto.
Wanachama wa Vikundi vya VICOBA wakiwa katika uzinduz wa utoaji wa mikopo ya uwezeshaji ambapo vikundi 272 vilipata mikopo toka Benki Posta (TPB) na Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo- UTT Microfinance Chini ya Udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8
yaani makala yote Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/vikundi-vya-vicoba-mikoa-ya-kanda-ya.html
0 Response to "Vikundi vya VICOBA Mikoa ya Kanda ya Ziwa vyapata mkopo wa Bilioni 2.8"
Post a Comment