Loading...

WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA

Loading...
WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA
link : WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA

soma pia


WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA

Wanafunzi wa Chuo cha Kodi (ITA) jijini Dar es Salaam, wametakiwa kutumia vyema teknolojia ya mawasiliano hususan mitandao ya kijamii kujifunza ili kupata maarifa badala ya kuitumia kwa mambo ambayo hayatawasaidia katika masomo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo wakati akiwakaribisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2017/18.Amesema vijana wengi wanatumia mitandao ya kijamii kwa masuala ya kijamii kwa kiwango kikubwa kuliko kuitumia kujifunza na kupata maarifa kwa mambo ambayo yatawasaidia kukuza kiwango cha elimu.

“Elimu ipo kila mahali siku hizi: katika vitabu, mitandao na tuna mambo mengi ambayo yanasaidia sana kujifunza tofauti na ilvyokuwa miaka 30 iliyopita. Ni wajibu wa wanafunzi kuitumia vyema mitandao hususan simu kujifunza na kupata maarifa”, alisema Prof. Jairo.

Mkuu huyo wa chuo amesema kwamba chuo cha kodi kinatumia mfumo wa kujenga umahiri kwa mwanafunzi ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi wa hali ya juu na ambao umelenga kumuwezesha mwanafunzi kujifunza badala ya kufundishwa. Ameongeza kwamba mfumo huo ndio utaratibu unaotumika ulimwenguni ili mwanafunzi anapohitimu awe na uwezo wa kujua nini cha kufanya katika fani yake na kwa Chuo cha Kodi ajue jinsi ya kukusanya kodi.
Wanafunzi wapya katika Chuo cha Kodi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo 
Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo (aliyesimama) akizungumza na wanafunzi wapya waliojiunga na Chuo hicho kwa muhula wa masomo wa kuanzia 2017/18. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Huduma za Fedha Emmanuel Foya na Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo Utawala, Fedha na Mipango Emmanuel Masalu. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs) 
Wanafunzi wapya katika Chuo cha Kodi wakifuatilia kwa makini maelezo ya Mkuu wa Chuo cha Kodi Prof. Isaya Jairo 




Hivyo makala WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA

yaani makala yote WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/wanafunzi-watakiwa-kutumia-mitandao.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO KUPATA MAARIFA"

Post a Comment

Loading...