Loading...

Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.

Loading...
Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.
link : Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.

soma pia


Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika Idara ya Utalii wameombwa kumpa ushirikiano Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Deograsius Mdamu, ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Wizara hiyo , Bi. Uzeeli Kiangi katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga baada ya kustaafu mwanzoni mwa mwezi Julai kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma akiwa ameitumikia Wizara kwa kushika nafasi mbalimbali kwa muda wa miaka 33.

Akizungumza katika hafla hiyo alisema ‘’ Watumishi ni kiungo muhimu katika kumsaidia Mkurugenzi wa Idara ya Utalii kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu kuwa mtampa ushirikiano katika hili’’

Amesema kupitia ushirikiano huo utasaidia kupelekea Wizara kutimiza azma ya kufikia watalii milioni 8 na fedha za kigeni dola bilioni 20 kila mwaka kufikia mwaka 2025.Aidha, Bi.Kiangi aliwataka watumishi kuzingatia miiko ya kazi zao kwa kutojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa wanapotimiza majukumu yao, la sivyo serikali hii ya awamu ya tano haitawaacha salama.

‘’Wakati wa utumishi wangu nilijitahidi kukwepa kupokea rushwa kwa kuwa sikujua huyu anayetaka kunihonga katumwa na nani na kwanini anipe rushwa wakati natimiza majukumu yangu jihadharini na watoa rushwa’’ alisisitiza
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye picha ya pamoja mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (katikati) katika hafla fupi ya kumuaga baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara Utalii, Bw. Deograsius Mdamu na Afisa Utalii Domina Moshi (kushoto)
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (kulia) akiwa na Afisa Utalii Mwandamizi, Martin Mrema (katikati) wakiwa wanatabasamu huku wameshika kwa pamoja moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha ya Bi. Kiangi aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu. 
Aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa kusimamia Sehemu ya Maendeleo ya Utalii katika Idara ya Utalii, Bi. Uzeeli Kiangi (Kulia) akiwa na Afisa Utalii Domina Moshi (katikati) wakiwa wanatabasamu huku Bi. Kiangi akiwa ameshika kwa moja ya zawadi ya saa ya mezani yenye picha yake aliyokabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki baada ya kustaafu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa Umma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Deograsius Mdamu.



Hivyo makala Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii.

yaani makala yote Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/11/watumishi-wa-wizara-ya-maliasili-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Watumishi Wa Wizara Ya Maliasili Na Utalii Wahimizwa Kutoa Ushirikiano ili Kukuza Utalii."

Post a Comment

Loading...