Loading...
title : ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU
link : ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU
ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU
Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu imefanya tamasha la ajira kwa kuwakutanisha waliokuwa wafanyakazi wa migodi hiyo na makampuni zaidi ya 20 kwa ajili kubalishana mawazo na kupeana mawasiliano na taarifa ili wafanyakazi hao wapate kazi.
Tamasha hilo limefanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika ukumbi wa Umoja uliopo katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo,Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu alisema lengo la tamasha la ajira lilioandaliwa na Acacia ni kuwaonesha fursa za ajira waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya Acacia kwa kuwakutanisha na makampuni mbalimbali katika kipindi cha kuelekea kufunga migodi hiyo.
“Tumekutana hapa ili kuonesha fursa za ajira kwa wafanyakazi wetu waliobobea katika kazi za migodini, kuna maisha mengine baada ya mgodi,tumealika kampuni ambayo yanachukua mawasiliano na CV na kama kuna nafasi za ajira basi watapatia ili maisha yaendelee nje ya mgodi”,aliongeza Busunzu.
“Tulialika makampuni zaidi ya 40, 15 yalikubali kushiriki,na 11 leo yamehudhuria,lakini pia wafanyakazi zaidi ya 260 wamehudhuria kwa ajili ya kuonana na makampuni haya,Acacia inaamini tamasha hili litakuwa na mafanikio makubwa tuliyotarajia”,alieleza.

Mgeni rasmi Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki akizungumza katika Tamasha la Ajira lililoandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia lililofanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika mgodi wa Buzwagi na kukutanisha pamoja makampuni zaidi ya 10 na wafanyakazi zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu wakati Acacia ikielekea kufunga migodi hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea lengo la kufanya tamasha la ajira lililokutanisha pamoja makampuni na wafanyakazi wa Acacia ili kupeana fursa za ajira. Kulia Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mganza,kushoto ni Dk. Chris Mauki.

Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akiwasisitiza waliokuwa wafanyakazi wa Acacia kutumia fursa ya tamasha hilo kutafuta maisha nje ya migodi.

Washiriki wa tamasha la ajira wakimsikiliza Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu .

Hivyo makala ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU
yaani makala yote ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/acacia-yafanya-tamasha-la-ajira-kuwapa.html
0 Response to "ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU"
Post a Comment