Loading...
title : DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA
link : DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA
DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA
Mkuu huyo wa wilaya amefanya ziara hiyo leo Jumamosi Disemba 2,2017 kwa ajili ya kujionea stadi za maisha na miradi mbalimbali inayofanywa na watoto wanaopata huduma katika vituo hivyo.Vituo vilivyotembelewa ni vituo vya Kanisa la ACT Shinyanga Mjini,AICT Kolandoto,TAG Shinyanga Mjini,PAG Shinyanga Mjini,KKKT Shinyanga Mjini.
Akiwa katika ziara hiyo,Matiro amejionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na watoto kama vile utengenezaji skonzi,biskuti,keki,nguo,mafuta,sabuni pamoja na ususi,ufumaji,saluni,ufyatuaji wa matofali,uchomeleaji wa vyuma,useremala,masomo ya kompyuta na mambo mengine kadha wa kadha.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,mkuu huyo wa wilaya alilipongeza shirika la Compassion kupitia makanisa yanayosimamia vituo hivyo ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwa watoto ambao wanajengewa uwezo wa kujiajiri.
“Nimegundua tuna jeshi kubwa la vijana wenye ujuzi wa aina mbalimbali,vijana tumieni fursa hii ya Compassion kujinufaisha kwa ajili ya maisha yenu,sisi kama serikali tunafarijika sana kuona vijana wakijengewa uwezo wa kujiajiri ili kuleta maendeleo katika jamii”,alieleza. Matiro alieleza kufurahishwa kuona jinsi vijana hao wanavyojengewa uwezo wa kutengeneza bidhaa mbalimbali na kuwashauri kuongeza jitihada ili kutengeneza viwanda kamili vya kutengeneza bidhaa.
“Sera ya serikali ni kuwa na viwanda,nimeona vijana wanatengeneza skonzi,biskuti kwa kutumia mashine za kisasa kabisa katika kituo cha AICT Ngokolo,hiki ni kiwanda,naomba kanisa na Compassion kwa kushirikiana na serikali tuangalie namna ya kupanua kiwanda hiki ili kuleta mabadiliko katika jamii na kitasaidia vijana kujikwamua kiuchumi”,alisema Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametembelea vituo sita vya huduma ya mtoto katika makanisa ya kiinjili yaliyo na ushirika na Compassion International Tanzania Klasa ya Shinyanga yenye vituo tisa.
Vijana wakimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro keki walizotengeneza.Vijana hao walisema wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza keki katika kituo hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia jinsi wanavyochomelea vyuma katika kituo cha kanisa la ACT Shinyanga mjini.
Hivyo makala DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA
yaani makala yote DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/dc-shinyanga-atembelea-vituo-vya-huduma.html
0 Response to "DC SHINYANGA ATEMBELEA VITUO VYA HUDUMA YA MTOTO VYA MAKANISA YENYE USHIRIKA NA COMPASSION KLASTA YA SHINYANGA"
Post a Comment