Loading...
title : DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI
link : DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI
DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), amekagua ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu-NBS mjini Dodoma na kutoa wito kwa wakandarasi wanaojenga miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo kutumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya Serikali na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Amesema hayo baada ya kushuhudia mkandarasi anayejenga jengo hilo Hainan International Ltd ya China, akitumia vifaa mbalimbali vya ujenzi vinavyopatikana hapa nchini zikiwemo mbao na vifaa vya umeme, hatua ambayo amesema inachangia kuwaongezea kipato wananchi.
Akizungumzia ujenzi huo, Dkt. Mpango amesema jengo hilo litatumika ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwakuwa litatumika kuchakata takwimu mbalimbali zitakazotumika katika kutunga sera na mipango mbalimbali ya kuendeleza nchi.
“Huwezi kupanga mipango yoyote bila kuwa na takwimu nzuri na bora, hapa ndipo vile “vichwa” vyetu vya takwimu nchini vitachakata takwimu hizo ndipo zitumike katika kutunga sera bora kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu” Alisistiza Dkt. Mpango
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), akitoa maelekezo wakati alipokagua ujenzi wa Jengo la ghorofa 5 la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa na kushoto kwake ni Mhandisi Mshauri Bw. Abdulkarim Msuya.
Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya (kulia) akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Mhandisi Mshauri na Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mjini Dodoma, Mhandisi Abdulkarim Msuya akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alipotembelea ili kukagua ujenzi wa Jengo hilo ambalo litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa, (wa tano kulia) mjini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI
yaani makala yote DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/dokta-mpango-awashauri-wakandarasi.html
0 Response to "DOKTA MPANGO AWASHAURI WAKANDARASI KUTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI KATIKA SEKTA YA UJENZI"
Post a Comment