Loading...

WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO

Loading...
WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO
link : WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO

soma pia


WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO

Na Said Mwinshehe, Globu ya Jamiii

MTOTO wa kwanza wa mwanamuziki Nguza Vicking, Nguza Mbangu amesema Mungu ameonyesha ukuu wake na kuifanya familia yao iliyokuwa kwenye kilio cha muda mrefu sasa kuwa kwenye shangwe. 

 Nguza ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Nabii Michael amesema hayo leo jijini Dar es Salaam nje ya gereza la Ukonga ambalo baba yake mzee Nguza alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kabla ya Rais Dk. John Magufuli kumuachia kwa msamaha wa Rais baada ya kutangaza kusamehe wafunga 8157 akiwamo mwanamuziki huyo na mwanaye Papii Kocha.

Nguza Mbangu amesema kilichotokea ni mapenzi ya Mungu kwa kuonesha ukuu wake huku akimshukuru Rais kwa kutoa msamaha huo, amesema familia itatoa tamko rasmi baada ya Rais kumtoa mzee wao kifungoni.  

 "Tutatoa tamko la familia kwa kilichotokea ila niseme tunamshukuru Mungu kwa kuonesha ukuu wake. Pia tunamshukuru Rais kwa uamuzi wake" amesema. 

Naye mwanamuziki maarufu King Kikii aliyekuwa nje ya gereza hilo baada ya kupata taarifa za kuachiwa Nguza Viking amesema kuwa kilio cha muda mrefu ambacho watanzania wamelia tangu Nguza Viking awe jela hatimaye imekuwa shangwe. Amesema  baada ya tamko hilo Nguza Viking amepigwa butwaa kwani haamin kama yupo huru lakini furaha imechukua nafasi yake.

Wakati huohuo mtoto wa kike wa Nguza Viking, Monica amesema anamshukuru Rais Mguful kwa kumtoa jela baba yake na kuongeza sasa furaha imerejea nyumbani. 

Nje ya gereza la Ukonga mashabiki wa mwanamuziki huyo wamejitokeza kwa wingi ili kumuona baada ya kuwa huru. Mara kadhaa baadhi ya askari magereza walizuia watu kusimama nje ya gereza hilo lakini watu waliamua kupiga kambi kuanzia saa saba mchana hadi jioni hii.


Hivyo makala WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO

yaani makala yote WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/watoto-wa-babu-seya-wamshukuru-rais.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATOTO WA BABU SEYA WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MSAMAHA KWA BABA YAO"

Post a Comment

Loading...