Loading...
title : JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI
link : JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI
JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI
Wanafunzi watano wa shule za serikali hapa nchini wameshinda shindano la uchoraji ambazo zinaeleza tukio halisi ambalo limetaribiwa na Jubilee Insuarance. Walioshinda wamepewa zawadi za bima za afya za jubilee insurance pamoja na kuahidiwa kushomeshwa elimu ya sekondari pindi watapofaulu.
Shindano hilo liliendeshwa kwa mikoa saba ambapo wanafunzi watano wameibuka kidedea baada ya kuchora picha hizo.
Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba ameishukuru Jubilee Insurance kwa kuanzisha shindano hilo ambalo limeweza kuwapa maisha wanafunzi watano kwa kuwa na uhakika wa afya zao pamoja na kusomeshwa elimu ya sekondari watapofaulu darasa la saba.
Amesema kuwa waendelee kuandaa mashindano mengi ambayo yatasukuma wanafunzi kushiriki kutokana na kuwa na uhakika wa zawadi.
Nae Mwenyekiti wa bodi wa Jubilee Life Corporation na Mwenyekiti wa Msaidizi wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Shabbir Abji amesema kuwa Jubilee Insuarance sasa imejikita katika kutoa huduma kwa jamii hasa kwa kaya maskini.
Mzazi wa Joseph Mwakyembe wa Mbozi mkoani Songwe, Joyce Mbuya amesema kuwa mtoto wake amemfanya kufika Dar es Salaam na kuwa na uhakika wa afya kupata bima ya afya ya Jubilee Insuarance.
Amesema kuwa Jubilee Insuarance imekuwa ya kwanza kuwafikia wananchi wa kawaida kwa kutafuta vipaji vya wanafunzi.
Mwenyekiti wa bodi wa Jubilee Life Corporation na Mwenyekiti wa Msaidizi wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Shabbir Abji akizungumza na wageni waalikwa kwenye utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda kwenye shindano la uchoraji wa michoro inayomuweka mtoto huru lililofanyaka hapa nchini.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba akitoa shukrani kwa Jubilee Insurance kwa kurudisha fadhira kwa jamii pamoja na na kuwasisitiza wajikite hasa kwa kaya maskini.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Jubilee Life Insuarence Corparition, Helena Mzena akitoa historia ya ya shindano lililoshirikisha shule za msingi mbalimbali hapa nchini kwenye shindano la uchoraji kwa wanafunzi wa darasa la Tatu wakati wa ugawaji wa zawadi kwa wanafunzi watano waliofanya vizuri.
Mkurugenzi Mkuu wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Dipankar Acharya akiwashukuru akizungumza jambo wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi waliofanya vizuri kwenye shindano la uchoraji.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA), Elia Kajiba akimkabidhi zawadi Mwanafunzi wa shule ya msingi Msasa, Khadija Mohamed Ali aliyeshinda kwenye shindano la uchoraji.
Meneja Mkuu wa The Jubilee Insuarance Company of Tanzania, Sumit Kumar Gaurav (kushoto) akimkabidi zawadi Mwanafunzi wa Shule ya msingi Katete, Atupele Wiston wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mashindano ya kuchora.
Hivyo makala JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI
yaani makala yote JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/jubilee-insurance-yatoa-zawadi-kwa.html
0 Response to "JUBILEE INSURANCE YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WATANO WALIOSHINDA SHINDANO LA UCHORAJI"
Post a Comment