Loading...
title : WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA
link : WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA
WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA
KAIMU Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Ndaki Barnabas amethibitisha kuwapokea majeruhi watatu ambao walijeruhuwa katika kata ya Bupu Wilayani Mkuranga na kundi la wafugaji wanao sadikika kuwa ni kutoka jamii ya wamang'ati waliowavamia jana jioni wakitokea katika eneo la Kisarawe Mkoani Pwani.
Dokta Ndaki amesema amewataja majeruhi hao kuwa ni Leonard Kondo, Mustafa Seif na Abdallah Rashid waliopokewa hospitalini hapo na kupatiwa matibabu majira ya saa nne usiku jana.
Dokta Ndaki anasema kuwa walipofikishwa hospitalini hapo hali za majeruhi hao zilikua mbaya na kuvuja damu lakini sasa wanaendelea vizuri baada ya kushonwa na kupata tiba ya awali huku akisema kuwa Daktari wa zamu amepita na kutoa ruhusa kwa majeruhi wawili huku majeruhi mmoja watampa rufaa ili aende kupata vipimo vya XRay na kipimo cha Ultra Sound sababu ameumia kwenye maeneo ya ndani ya mwili ikiwemo mbavuni na ana maumivu makali.
Wakizungumza na globu ya jamii mchana huu wakiwa wodini wagonjwa hao wameelezea namna walivyovamiwa na kupigwa vibaya na wafugaji hao.
Akizungu huku akiwa kitandani majeruhi Abdallah rashid ambaye ni mkazi wa Mbagala amesema akuwa yeye alikwenda Kisarawe kuwasalimia wakwe zake na kadhia hiyo ilimkuta wakati alipokwenda dukani kununua vocha ndipo ghafla wakatokea wamang'ati huku wakimuuliza kama ameonga ng'ombe aliyekatwa mguu akajibu hajaona ghafla wakamvamia na kuanza kumpiga kwa kutumia gongo kichwani.
"Nikawaona wenyeji wanakimbia na mimi nikaona hapo sasa kuna hatari nikakimbia nankwenda kujificha kwenye nyumba nikapata akili ya kumpigia Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lkn akasema yeye hivi sasa ameshahamishwa hivyo akaniambia nimpigie RPC mpya wa sasa nikafanya hivyo Kamanda wa sasa alipokea simu na kuniambia ndani ya nusu saa askari watakuwa wamefika kutuokoa kweli walifika ndani ya muda na wakatuchukua kutupeleka hosputali" anasema majeruhi huyo.
Tukio limethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Philiberto Sanga huku akiahidi kuwa kesho ataambatana na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Mkuranga kwenda katika eneo la tukio.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Madiwani na wananchi waanzishe daftari la kuwaandika wageni wanaoingia nankutoka katika maeneo yao ili kudhibiti vitendo viovu.
Hivyo makala WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA
yaani makala yote WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/wamangati-wawajeruhi-watatu-mkuranga.html
0 Response to "WAMANG'ATI WAWAJERUHI WATATU MKURANGA"
Post a Comment