Loading...

JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION

Loading...
JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION
link : JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION

soma pia


JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION

DODOMA: Shirika la LEAD Foundation linalojihusisha na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira limezindua mradi wa Kisiki Hai Mkoa wa Dodoma wenye lengo la kukomboa ardhi iliyochakaa ya mashamba na malisho ili kupambana na baa la njaa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa ufunguzi wa mradi huo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la LEAD Foundation, Mhandisi Njamasi Chiwanga amesema kuwa lengo la Mradi wa Kisiki Hai ni kuhakikisha wanafikia jumla ya kaya laki moja na themanini (180,000) ambazo zipo katika hali mbaya ya mazingira ziweze kutunza hekta 180,000 kwa kustawisha miti milioni 14 kwa njia ya Kisiki Hai (FMNR - Farmer Managed Natural Regeneration) ifikapo mwaka 2020.

Njamasi amesema kuwa mikakati waliyonayo katika mradi huo ni pamoja na kujenga mshikamano wa wadau wote wa mazingira hususan viongozi wa wilaya, wakuu wa idara na taasisi mbalimbali, madiwani, watendaji wa kata pamoja na viongozi wa dini ili kuweza kushirikiana katika kufanikisha kukomboa mazigira. Kwa kuanzia mradi unatarajia kunufaisha tarafa mbili zilizo athiriwa zaidi na uharibifu wa mazingira katika kila wilaya ili kufikia nusu ya kaya zote za Mkoa wa Dodoma.

Mgeni Rasmi katika ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Deo Ndejembi amesema anaunga mkono mradi huo na atahakikisha unafanikiwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbalimbali watakayo hitaji katika kufanikisha mradi huo.Kwa upande wao baadhi ya wadau waliofika katika ufunguzi wa mradi huo wamesema kuwa mpango wa Kisiki Hai ni mzuri na wana hakika iwapo wananchi wataupokea vizuri baada ya muda mfupi changamoto ya uharibifu wa mazingira katika Wilaya ya Kongwa itakuwa ni historia.

Kisiki Hai ni mradi wa miaka mitatu na unatarajiwa kufikia Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na kwa sasa umenza katika Wilaya ya Kongwa ambapo umeanza na tarafa ya Kongwa na Mlali za wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi akifungua rasmi mradi wa LEAD Foundation.

 Mkurugenzi wa Programu - LEAD Foundation Mhandisi Njamasi Chiwanga akiwasilisha mpango wa Programu
Wadau walio hudhuria warsha ya mazingira ya Kisiki Hai



Hivyo makala JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION

yaani makala yote JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/jumla-ya-kaya-180000-kufikiwa-na-mradi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JUMLA YA KAYA 180,000 KUFIKIWA NA MRADI WA LEAD FOUNDATION"

Post a Comment

Loading...