Loading...

TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO

Loading...
TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO
link : TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO

soma pia


TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO

Na John Mapepele 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilano, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (0784 441180).

Tanzania na Uganda leo wamekubaliana kuunda mara moja timu ya pamoja ya wataalamu wa mifugo itakayokuwa ikifuatilia hali ya mifugo ili kudhibiti milipuko ya magonjwa hatari ya Mifugo.

Akizungumza leo mjini Bukoba kwenye mkutano wa wataalam wa mifugo wa Tanzania na Uganda ulioandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini, Balozi wa Uganda nchini bwana Richard Tumusiime Kabonero amesema ushirikiano wa karibu baina ya Tanzania na Uganda kwenye sekta ya mifugo siyo kitu cha hiari bali ni jambo la laziima ili kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari kwa mifugo ya pande zote mbili.

Balozi Kabonero amesema njia bora ya kudhibiti magonjwa ya wanyama ni kuwa na timu ya pamoja ya wataalam watakaokuwa wakifuatilia hali ya mifugo na kufanya tathmini kila wakati badala ya utaratibu wa sasa wa kila nchi kushughulikia peke yake.“Uganda kama ndugu wa karibu wa Tanzania tuna kila sababu ya kushirikiana ili kuboresha sekta hii” alisisitiza balozi Kabonero

Akizungumzia kwa upande wa Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo amesema ushirikiano huo utasaidia kuboresha huduma za mifugo baina ya nchi mbili kwa kuzingatia kuwa taaluma ya udaktari wa mifugo imehuishwa na inadhibitiwa na bodi za taaluma hiyo kidunia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo(aliyeshika fimbo) akipima kina cha KIsima kilitengenezwa kienyeji kwa ajili ya kunyweshea mifugo katika eneo la Kafunjo Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera leo. Waliomzunguka ni wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifana Halmashauri ya Missenyi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mikono) akiongea na wafugaji wa nchini Uganda leo baada ya kufanya ziara ya kikazi katika eneo la Omwaarogwamabaare. Kushoto ni Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Tanzania, bwana Richard Tumusiime Kabonero kulia (anayecheka) ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Martin Ruheta. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo, Dkt. Mary Mashingo (aliyenyanyua mkono)akimweleza jambo Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe.Richard Tumusiime Kabonero (kulia) walipokuwa katika ziara ya kikazi leo kwenye Mto Kagera katika kijiji cha Kakunyu. Wengine kushoto kwa Katibu Mkuu ni Dkt. Martin Ruheta Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kulia kwa Balozi ni Suleiman Ahmed saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.



Hivyo makala TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO

yaani makala yote TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/tanzania-na-uganda-waunda-timu-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TANZANIA NA UGANDA WAUNDA TIMU YA WATAALAMU KUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO"

Post a Comment

Loading...