Loading...

Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza

Loading...
Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza
link : Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza

soma pia


Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela amewataka madereva wanaoendesha magari ya zimamoto na uokoaji kwenye viwanja vyote vya ndege Tanzania kuyathamini na kuyatunza magari hayo kwa kuwa wameaminiwa kufanya kazi hiyo.

Bw. Mayongela alitoa kauli hiyo kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), alipokwenda kujitambulisha na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili, ambapo alisema magari hayo yamenunuliwa kwa gharama kubwa, hivyo yanapaswa kutunzwa.

Alisema uthamini wao kwa magari hayo kutayafanya kudumu na kuyafanya kazi kwa muda mrefu bila kuharibika, jambo ambalo litachangia ufanisi wa kazi, ya uokoaji na usalama kwenye viwanja vya ndege, ambapo mbali na miundombinu pia lazima miundombinu ipewe kipaumbele.

“Najua wapo wenzenu wachache sio waaminifu wamekuwa wakitengeneza manunuzi hewa ya vifaa na hata mafuta kwa manufaa yao binafsi, lakini ninawaomba mujione nyie ndio wenye thamani kwa kuaminiwa kuendesha magari haya ya mamilioni ya fedha, kwani ni nyie tu mnayoweza kuyaendesha kutokana na kuwa na mitambo ya kisasa tofauti kidogo na mengine, hivyo basi tuyatunze ili tuisaidie serikali yetu isiingie gharama za mara kwa mara za kununua vifaa au magari mengine mapya,” alisisitiza Bw. Mayongela.

Hatahivyo, alisema zimamoto ni moja ya mambo ya msingi hivyo amewahakikishia kuwapeleka kozi za mara kwa mara za ndani na nje ya nchi, kutokana na mambo mbalimbali yanayobadilika duniani, na kwa kuanzia ataanza na askari wawili hadi wanne, kulingana na mafunzo wanayostahili kushiriki, na atahakikisha washiriki ndio wanaokwenda kufanyia kazi kwa vitendo katika utendaji wao na sio kupeleka mabosi ambao hawahusiki.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (aliyesimama mbele), akiongea na askari wa zimamoto na uokoaji wa kituo cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Mbele kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Bw. Johannes Munanka na (kulia) ni Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji wa Viwanja vya Ndege nchini, Kamishna Msaidizi, Christom Manyologa.

Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (aliyesimama mbele) akitoa maelezo mbalimbali kwa askari wa zimamoto na uokoaji katika kikao kilichoitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna Msaidizi, Christom Manyologa (aliyesimama) akiongea na askari wa kituo cha zimamoto na uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, katika mkutano ulioitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela.



Hivyo makala Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza

yaani makala yote Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kaimu-mkurugenzi-taa-ataka-madereva-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kaimu Mkurugenzi TAA, Ataka Madereva Wa Magari Ya Zimamoto kuyatunza"

Post a Comment

Loading...