Loading...
title : WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO
link : WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO
WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Wanafunzi wanaoomba Mikopo ya Elimu ya Juu wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu Juu (HESLB) ili kuweza kurahisisha katika uchambuzi.
Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati wa tathimini na changamoto za waombaji wa Mikopo ya Elimu Juu kwa kushirikiana Shirika laPosta , Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala Usajili Udhamini na Ufilisi (RITA) pamoja na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), amesema kuwa wanafunzi wakifuata taratibu zilizowekwa kunapunguza changamoto katika uchambuzi wa mikopo.
Amesema kuwa nyaraka zote zinazohitajika na bodi ni muhumu hivyo waombaji lazima wazingatie wanaweka vigezo vilivyowekwa na bodi ya mikopo na wasipoweka vigezo hivyo fomu inakuwa haijakamilika.
Aidha amesema kuwa wanafunzi ambao hawajaomba waendelee kuomba katika kipindi hiki kilichobaki ili wasiweze kuachwa katika utaratibu huo.
Wakala Usajili Udhamini na Ufilisi (RITA) imesema kuwa wanafunzi waliomba vyeti vya kuzaliwa 41573 tangu walipoanza utaratibu wa kutoa vyeti kuzaliwa na vifo kwa wanafunzi hao na utaratibu huo vyeti 25676 uko tayari vimepitishwa.
Akizungumzia changamoto za uombaji Mkurugenzi Tehama, Cuthbert Simalenga amesema kuwa wanafunzi wengine wamekuwa na weka picha ambazo haziko katika taratibu za uombaji uliowekwa.
Shirika la Posta Nchini (TPC) limesema kuwa jumla ya fomu za maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu 14440 ambayo yaliombwa na wanafunzi hao, fomu 12823 wameziwasilisha bodi ya Mikopo na fomu 1619 ziko katika mchakato wa kuzisafirisha.
Akizunguma katika tathimini ya waombaji wa mikopo, Meneja Mkuu wa Uendesha wa Shirika la Posta (TPC)Mwanaisha Said amesema kuwa wazazi wawape fedha mapema wanafunzi wanaomba mikopo katika bodi katika kuondoa changamoto.
Mkurugenzi Mtendaji HESLB, Abdul-Razaq Badru akizungumza katika tathimini ya waombaji wa mikopo katika bodi hiyo na changamoto ambazo wanakumbana nazo na taasisi zinazohusika katika maombi hayo.
Mkurugezi wa Tehama wa RITA, Cuthbert Simalenga akizungumza kuhusiana na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa waombaji wa katika bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu.
Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa Shirika la Posta Nchini (TPC) , Mwanaisha Said akizungumza kuhusiana na usafirishaji wa fomu za wanafunzi wanaomaba mikopo katika bodi ya mikopo.
Picha pamoja kwa watendaji wa taasisi zinazohusiana na katika uombaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Picha pamoja kwa watendaji wa taasisi zinazohusiana na katika uombaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na wanafunzi waombaji wa mikopo
Hivyo makala WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO
yaani makala yote WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/wanafunzi-watakiwa-kufuata-taratibu-za.html
0 Response to "WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO"
Post a Comment