Loading...

KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA

Loading...
KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA
link : KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA

soma pia


KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA

 Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar Johari M. Sururu amewataka Askari na Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji kufanyakazi kwa Uweledi na kujituma ili kuweza kutekeleza vyema majukumu yao ya msingi ya kusimamia na kudhibiti Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Watu Nchini. “Ili kuimarisha utendaji wetu ni vyema kuacha kufanya kazi kwa mazoea na muda wote, tutoe huduma za Uhamiaji bila ya Upendeleo, Unyanyasaji au Ucheleshwaji usio wa lazima. Tumieni lugha nzuri, zingatieni kwa vitendo dhana ya kumjali Mteja na Epukeni vitendo vya Rushwa wakati mkitoa huduma mbali mbali za Uhamiaji kwani Rushwa ni Adui nambari moja wa Haki” alisema Kamishna Sururu.
Kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ndio mhimili mkuu wa mafanikio ya Taasisi yoyote ile ikiwemo ya Uhamiaji. Maafisa na Askari wa Uhamiaji wanapaswa kuheshimu na kutii Kanuni zote za kijeshi, “Idara yetu imeingia rasmi kwenye mfumo wa Kijeshi nasi hatuna budi kufanyakazi kwa Kasi, Ari na Mori kuhakikisha kwamba jukumu la Ulinzi na Usalama wa Mipaka ya Nchi yetu linatekelezwa ipasavyo” alisema hayo wakati akizungumza na Askari na Maafisa wa Uhamiaji waliopo Mkoa wa Kaskazini Pemba, akihitimisha ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba iliyoanza tarehe 18 – 21 Disemba, 2017. 
Aidha katika ziara hiyo, Kamishna Sururu alipata fursa ya kutembelea maeneo mbali mbali yenye changamoto za uwepo vipenyo na Bandari Bubu zinazotumiwa na wakaazi wa maeneo hayo, kwa shughuli mbali mbali zikiwemo za uvuvi na biashara, baina ya visiwa vya Pemba na Mombasa, Kenya. Kisiwa cha Pemba kinasemekana kuwa na Bandari bubu zaidi ya mia tatu (300) ambapo inaelezwa kuwa ni kimbilio kwa baadhi ya Raia wa Kenya na Raia wa Somalia ndani ya visiwa vidogo vidogo vilivyomo ndani ya Wilaya za Micheweni, Wete na Mkoani, Pemba. 

Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari M. Sururu akipokea salamu kutoka kwa Askari wa Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwasili Ofisi hapo kwa ziara ya kikazi Mkoani humo tarehe 20 - 21 Disemba, 2017. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha.

Kamishna Sururu aliwasisistiza Askari wa Uhamiaji kuongeza Doria na Misako ili kuwabaini wale wote wanaojipenyeza na kuishi nchini kinyume cha Sheria za Uhamiaji nchini. “Pamoja na changamoto zilizopo kutokana na Jiografia ya Visiwa vya Unguja na Pemba, hatuna budi kusimamia vyema jukumu la Udhibiti wa Ungiaji na Utokaji wa Watu” “Kama mnavyoelewa jitihada mbali mbali zinazochukuliwa na serikali zetu zote mbili katika kuboresha utendajikazi wetu, Idara inatarajia kupata vitendeakazi pamoja na vyombo vya usafiri yakiwemo Magari na Pikipiki, ambavyo vitasaidia kuboresha utoaji wa huduma zetu kwa Jamii” alifafanua Kamishna Sururu.

Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Said M. Samaki akichangia hoja katika kikao cha pamoja na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar na Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 


Hivyo makala KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA

yaani makala yote KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kamishna-wa-uhamiaji-zanzibar-atangaza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR ATANGAZA NEEMA"

Post a Comment

Loading...